Home » » Sekta ya afya Rukwa hoi

Sekta ya afya Rukwa hoi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

SEKTA ya afya mkoa wa Rukwa inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu mkubwa wa kada za kitaalamu ambapo uwiano uliopo daktari mmoja analazimika kuhudumia wagonjwa 200,000 kwa mwaka.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Dk Hans Ulaya alisema idadi hiyo ya wagonjwa ni zaidi ya mara nane ya uwiano wa Kitaifa, ambapo daktari mmoja anahudumia wagonjwa 25,000 kwa mwaka.
Dk Ulaya alibainisha hayo wakati wa kikao cha Ushauri wa mkoa wa Rukwa (RCC) kilichofanyika juzi mjini hapa chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Magalula Said.
Aliongeza kuwa uhaba wa kada za kitaalamu pia umewakumba wauguzi ambapo muuguzi mmoja mkoani humo analazimika kuhudumia wagonjwa 30,000 kwa mwaka, ikiwa ni mara sita zaidi ya uwiano wa kitaifa ambapo muuguzi anahudumia wagonjwa 5,000 tu kwa mwaka.
Dk Ulaya alisema sekta hiyo pia inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vituo vya afya vya kutolea huduma ya afya vipatavyo 188 ukilinganisha na idadi ya kata na vijiji vilivyopo.
Akifafanua alieleza kuwa changamoto nyingine kubwa ni halmashauri ya Sumbawanga na Kalambo hazina hospitali hivyo hutumia hospitali ya mkoa kama ya wilaya na kwamba kata zipatazo 77 hazina vituo vya afya na vijiji 153 havina zahanati.
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa mkoa wa Rukwa una idadi ya kata zipatazo 97 na vijiji 341, ambapo idadi ya vituo vya afya ni 20 tu na zahanati zikiwa 179. Kwa mujibu wa Magalula ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa watumishi wenye taaluma mkoa unajitahidi kuwaendeleza kitaalamu watumishi wachache waliopo na kuomba vibali vya kuajiri watumishi wapya.

Chanzo: Habari Leo
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa