Home » » MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YA WANUFAISHE WATANZANIA

MADINI YOTE NCHINI NI SHARTI YA WANUFAISHE WATANZANIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Aliyenyoosha mkono) akimuonyeshaNaibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko mitambo ya uchimbaji madini  alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe alipotembelea mgodi wa Edenville Tanzania Ltd uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.
Mhandisi Joseph Mwakabage Meneja Mradi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe (Kulia) akimueleza Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko juu ya uchimbaji wa makaa ya mawe alipotembelea mgodi huo uliopo Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kikzai Mkoani Rukwa, Leo 23 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Rukwa

Serikali imesema kuwa sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza wazi kuwa Madini yote nchini ni Mali ya watanzania hivyo wanapaswa kutambua umuhimu wa rasilimali.

Wawekezaji na wachimbaji wote wa madini nchini wanapaswa kutambua kuwa wanalo jukumu muhimu la kurejesha kwa jamii asilimia chache ya kile wanachozalisha kwa kuunga mkono juhudi za serikali Back to the Community) katika kuboresha miundombinu, sekta ya elimu, afya N.K

Naibu Waziri wa Madini nchini Mhe Doto Mashaka Biteko amesisitiza hayo Leo 23 Februari 2018 wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkomola 2, Kata ya Kipande, Wilayani Nkasi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe Mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania.

Mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Edenville Tanzania Ltd kwa ubia na kampuni ya Edenville Energy of Uk na Upendo Group (Kampuni ya kizawa) ilianza shughuli za majaribio ya uchimbaji na uoshaji mwezi wa kumi mwaka Jana 2017 na mkaa wa kwanza kuuzwa kwa majaribio ni mwezi Novemba mwaka 2017.

"Nataka niwajulishe tu watanzania wenzangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliniteua kusimamia Wizara ya Madini nikimsaidia Waziri wetu Mhe Anjelina Kairuki ili kuboresha sekta hii ya Madini hatimaye kuwanufaisha watanzania kuliko ilivyokuwa awali ambapo Madini yalikuwa yanachimbwa nchini lakini faida inaenda nchi zingine" Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa

Wawekezaji hao wanapaswa kutoa ajira zisizo za utaalamu kwa wananchi wanaozunguka migodi yao sambamba na watanzania wote huku akiwaagiza kuwaajiri wataalamu wa Madini wa ndani ya nchi kwa kazi ambazo wanaweza kuzifanya sio kuajiri wageni.

Aidha, aliwasisitiza wananchi hao pindi wanapopata ajira zao katika migodi mbalimbali wanapaswa kuwa waaminifu ili kuwavutia wawekezaji hao jambo litakalopelekea wawekezaji kuwa na imani na watanzania na hatimaye kuongeza chachu ya ajira nyingi zaidi.

Sambamba na hayo amekemea baadhi ya wafanyakazi katika migodi mbalimbali ambao wameaminiwa na kupatiwa ajira lakini wanageuza muda wa kazi kuwa muda wa starehe kwa kunywa pombe na utoro kazini.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Rukwa kutembelea na kukagua uchimbaji wa Madini.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa