Home » » RUKWA KUPATA UMEME WA UHAKIKA : JIWE LA MSINGI LAWEKWA KATIKA MRADI MKUBWA

RUKWA KUPATA UMEME WA UHAKIKA : JIWE LA MSINGI LAWEKWA KATIKA MRADI MKUBWA

Na Khadija Dalasia
Mkoa wa Rukwa unatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dr.Dotto Mashaka Biteko, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Kilovoti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia ambao utaunganisha Bara la Afrika kutoka Afrika Kusini hadi Ethiopia.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi mradi huo wa TAZA iliyofanyika leo, Julai 29, 2024, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Kata ya Malangali, Mheshimiwa Dr. Biteko amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia takribani shilingi bilioni 15 kila Mwaka kununua umeme kutoka nchi jirani ya Zambia kwa ajili ya kuhudumia Mkoa wa Rukwa.

Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu amebainisha kuwa hatua ya kuunganishwa kwa Mkoa wa Rukwa katika gridi ya Taifa itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kuvutia uwekezaji zaidi katika viwanda vya kuchakata na kusindika mazao hasa kwa kuwa Mkoa wa Rukwa ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo.

Aidha Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu ametoa maagizo kwa Mkandarasi wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) kuhakikisha kuwa umeme unawashwa katika vijiji 30 ambavyo bado havijafikiwa ifikapo Agosti 30, 2024.

 

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa