Home » » KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI.

KIWANJA CHA NDEGE SUMBAWANGA CHAFIKIA ASILIMIA SITINI YA UJENZI.

Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga umefikia asilimia sitini ya utekelezaji wake. 

Taarifa hiyo imetolewa mbele waandishi wa habari leo Machi 26, 2025 na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Joseph Jimonge.

Ameeleza kuwa mradi huo unaogharimu bilioni 60 unatarajia kukamilika Juni 2025.

Mhandisi Jimonge ameeleza kuwa ujenzi wa kiwanja hicho unalenga kuimarisha uchumi kwa kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji Mkoani hapa na kuwa kichocheo cha kufunguka kwa fursa mpya za kibiashara.

"Kiwanja cha ndege cha Sumbawanga kitaleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa Mkoa wa Rukwa. Zaidi ya abiria 150,000 watapata huduma za usafiri wa anga kila Mwaka, na hii ni fursa kubwa kwa wajasiriamali, wakulima, na wafanyabiashara wa Mkoa wetu," ameeleza Mhandisi Jimonge.

Mbali na kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji, mradi huo unatarajia kutoa pia ajira kwa wakazi wa Rukwa, hasa katika sekta za ujenzi, usafiri wa ndani ya Mkoa, na huduma nyingine za kijamii. 

Aidha, uwanja huo unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wakazi wa mikoa ya jirani, ambao walikuwa wakilazimika kusafiri zaidi ya kilomita 300 kufuata huduma za usafiri wa anga katika mikoa mingine.

Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafiri katika maeneo mbalimbali nchini, kama sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi wa viwanda, biashara, na maendeleo ya jamii. 

Mradi wa kiwanja cha ndege cha Sumbawanga ni mfano mwingine wa dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa kila Mkoa unafaidika na miundombinu ya kisasa inayochochea maendeleo ya haraka.





Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa