Home » » CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA

CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUKWA CHARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA MANISPAA YA SUMBAWANGA

Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa ikiongozwa na Hajjat Silafu Jumbe Maufi, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Rukwa imeridhishwa na ubora wa miradi inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Rukwa imeanza ziara ya siku nne katika Halmashauri za Mkoa wa Rukwa ikikagua  utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 -2025 katika Mkoa wa Rukwa kuanzia tarehe 24 Julai hadi tarehe 27 Julai 2024.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Rukwa wamekagua utekelezaji wa miradi  8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.1 katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Miradi iliyokaguliwa ni  ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Senga, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa Shule ya Msingi Wipanga, ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Sumbawanga Asilia.

Miradi mingine iliyotembelewa na kukaguliwa ni ujenzi wa Wodi  Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga - Isofu, ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mazoezi Kata ya Chanji, ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Sokolo Kata ya Kizwite , ujenzi wa  vyumba vya madarasa sita na matundu nane  ya vyoo katika Shule ya Sekondari Lwiche na ujenzi wa Vyumba tisa vya Madarasa  na matundu vyoo 8  katika Shule ya Sekondari Kizwite.

Kamati imeitaka Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kuweka katika mipango na bajeti fedha kwa ajili ya kuzijengea uzio Shule zote ili kuimarisha ulinzi  kwa wanafunzi  na kuzuia uvamizi wa maeneo ya Taasisi za umma.



Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa