Mwanafunzi
wa darasa la nne katika shule ya msingi Swaila, kata ya Mkwamba
wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Maria Pangani (14) amekufa papo hapo baada
ya kupigwa radi.
Mwanafunzi
huyo aliyekuwa akisoma kupitia Mpango wa Memkwa, alipigwa na radi akiwa
amejificha porini baada ya mama yake kumtishia kuwa atafikishwa katika
Serikali ya kijiji hicho baada kugundua kuwa alikuwa akiimiliki kwa siri
simu ya kiganjani bila kufahamika aliyemnunulia.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarunda alithibitisha tukio hilo na
kueleza kuwa lilitokea Machi 22 , saa 11:00 jioni katika kijiji cha
Swaila wilayani Nkasi.
Akizungumzia
mkasa huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Swaila, Juvenary Mmanzi alisema,
mama mzazi wa mtoto huyo alishangaa kuona binti yake akiwa na simu.
“
Ndipo mama yake alipomhoji alikoipata simu hiyo, binti alikataa kumtaja
mtu aliyemnunulia ndipo mama yake alipohamaki na kumtishia kuwa
atampeleka katika Serikali ya Kijiji afungwe asipomtaja mtu
aliyemnunulia simu hiyo “ alieleza Mmanzi.
Kwa
mujibu wa Mmanzi, mtoto huyo alijawa na hofu kubwa ya kufungwa jela
akakimbilia porini kujificha na ghafla mvua ilianza kunyesha na ndipo
alipigwa na radi.
Inadaiwa kuwa, wakazi wa kijiji hicho walifika kwenye pori hilo na kukuta mwili wa marehemu ukiwa umeunguzwa.
Simu na matunda aina ya mapera vilikutwa kwenye mfuko wa sketi aliyokuwa ameivaa.
Kwa
mujibu wa Mwaruanda, uchunguzi wa kitabibu umeonesha kuwa kifo cha
mtoto huyo kimesababishwa na radi iliyompiga, mwili wake ulikabidhiwa
kwa wazazi wake kwa maandalizi ya maziko.
Kijukuu cha Bibi K
0 comments:
Post a Comment