Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga
mjini, Aeshi Hilaly (CCM) aliyoifanya katika Hifadhi ya Msitu wa Mbizi
juzi. Alibaini ‘mchezo mchafu’ ulioisababishia halmashauri hiyo hasara
hiyo ikiwa ni tozo iliyotakiwa kuilipa baada ya uvunaji na mauzo ya
magogo ya msitu huo kufanyika.
Hifadhi ya Msitu wa Mbizi kiko umbali wa kilometa 12 kutoka mjini
Sumbawanga ukiwa ni chanzo kikuu cha maji kwa asilimia zaidi ya 80, uko
chini ya TFS. Meneja wa Hifadhi ya Msitu wa Mbizi, Mohamed Kihangi
alieleza kuwa TFS iliiruhusu Taasisi ya Utafiti wa Misitu nchini
(TAFORI) ambayo iliuzia kampuni binafsi ya Daloshebedea General Ltd ya
Iringa ambayo ilivuna katika hekta sita za magogo kwenye msitu huo yeye
thamani zaidi ya Sh milioni 100.
Kihangi alieleza kuwa aliishirikisha Manispaa katika hatua zote za
uvunaji wa msitu huo uliofanyika kwa zaidi ya miezi mitatu huku Manispaa
kukana na hawakuwa na taarifa hiyo hadi dakika za mwisho.
Ofisa Misitu wa Manispaa ya Sumbawanga, Joseph Nkonjera awali alikana
kushirikishwa katika uvunaji wa magogo katika msitu huo isipokuwa
katika hatua za mwisho za uvunaji.
Pia hana taarifa ya ukubwa wa eneo la msitu uliovunwa.
Ndipo Mbunge Hilaly alipombana kwa kumtaka aeleze ukweli kwa kuwa
haingii akilini magogo kuweza kusafirishwa kutoka mjini Sumbawanga hadi
Iringa bila kuwa na vibali kutoka Ofisi ya Maliasili ya manispaa hiyo.
Nkongera alikiri kuwa alipokea ushuru wa Sh 900,000 kati ya milioni
50 zilizopaswa kulipwa na kampuni ya Dalashebedea General Ltd ya Iringa.
Kutokana na hilo, Mbunge huyo alimtaka Meneja wa Hifadhi ya Misitu ya
Mbizi, Kihangi kuwasiliana na TFS , TAFORI na Kampuni ya Daloshebedea
kuwasilisha vielelezo vya uvunaji na manunuzi magogo hayo ili waweze
kujua ni namna gani manispaa hiyo itapata haki yake kutokana na uvunaji
huo.
Pia wamemtaka Ofisa Misitu wa Manispaa hiyo , Nkojera kuwakilisha
stakabadhi za manunuzi na malipo ya tozo alizopokea kutoka kampuni
binafsi ya Daloshebedea General Ltd.
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment