Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Taasisi ya Benjamini Wiliam Mkapa imekabidhi nyumba 19 kwa Halmashauri za Mikoa ya Katavi na Rukwa kwa ajiri ya watumishi wa Idara ya afya zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Biloni 1.3.
Makabidhiano ya nyumba hizo yalifanyika juzi
katika zahanati ya Kabungu Wilayani Mpanda kwaniaba ya nyumba nyingine
zilizojengwa katika Halmashauri za mikoa ya Katavi na Rukwa ambapo mgeni
Rasmi alikuwa Waziri Mkuu msitaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda.
Katika Risara iliyosomwa na Asifa Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Benjamini Wiliam Mkapa Dkt Ellen Senkoro alisema wakati taasisi hiyo inaadhimisha miaka kumi ya kazi zao wamechangia jitihada mbalimbali za Serikali hapa nchini ikiwemo mikoa ya Rukwa na Katavi.
Alisema mbali ya ujenzi wa nyumba hizo za watumishi wa afya pia Taasisi hiyo imeajiri watumishi 63 na kuwapeleka katika mikoa hiyo miwili ambao wamekuwa wakitowa huduma za tiba na maabara katika Hospitali na vituo vya afya vya Serikali .
Pia wameimarisha vyuo vya mafunzo vya afya kwa kuajiri na kupeleka walimu 8 katika vyuo vilivyopo katika Mkoa wa Rukwa kwa nia ya kuhakikisha vyuo hivyo vinapata uwezo mkubwa zaidi wa kudaili na kufundisha wanafunzi wa kada za afya nia kuongeza uzalishaji zaidi ya wataalamu wa afya nchini.
Dkt Senkoro alisema kuhusiana na mradi huo wa ujenzi wa nyumba Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia Wazee na Watoto waliamua kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Mkapa katika kutekeleza mradi kuanzia mwaka 2011 hadi 2016 mradi huo unalenga kuimarisha mfumo wa sekta ya afya .
Alisema Taasisi hiyo mpaka sasa imejenga nyumba 480 hapa nchini kati ya nyumba hizo nyumba 40 zipo katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
Waziri Mkuu msitaafu Mizengo Pinda alitowa shukurani kwa Taasisi ya Mkapa kwa kuratibu na kupatikana kwa msaada huo mkubwa .
Pinda alisema Serikali yetu licha ya mafanikio yaliyopatikana nchi yetu bado inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa watumishi wa afya hasa vijijini nale yasiyofikika kwa urahisi .
Pia aliwataka watumishi wanaopangiwa kazi katika mikoa ya Katavi na Rukwa kuacha imani potofu kuwa mikoa hiyo inauchawi hari ambayo imepelekea watumishi wanaopangiwa kazi kushindwa kulipoti.
Muuguzi wa Zahanati ya Kabungu Rose Mpimbe alisema nyumba
waliyokadhiwa itawafanya wananchi wa Kata ya Kabungu kupata huduma kwa
muda wote kwani walikuwa wakishindwa kutowa huduma kwa wagonjwa kutokana zahanati
hiyo kutokuwa na nyumba ya kuishi mganga wala wauguzi ambao wote
walikuwa wamepanga nyumba kijiji cha jirani cha Kagwila kilichopo umbali
wa kilimeta mbili
0 comments:
Post a Comment