Home » » Elimu ya afya ya uzazi chachu ya kupunguza vifo vya wajawazito.‏

Elimu ya afya ya uzazi chachu ya kupunguza vifo vya wajawazito.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Walter  Mguluchuma
Sumbawanga.

 JAMII kutofahamu haki za msingi za afya ya uzazi na mifumo dume ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo vya wanawake wajawazito katika mikoa ya mbalimbali hapa nchini, imefahamika.

Meneja Mradi wa shirika la Swedish Association for Sexuality Education (RFSU) Cuthbert Mendaenda,alisema hayo wakati akizungumza kwenye kikao wakuu wa vyuo mbalimbali kilicholenga kuwafahamisha kuhusu mradi wa Tanzanian Men as Equal Partners (TMEP), kilichofanyika jana  kwenye ukumbi wa Libori mjini hapa.

Alisema kuwa utafiti waliofanya wamebaini kuwa wananchi wengi hasa vijijini hawajui haki za msingi za afya ya uzazi hivyo kuipa mwanya mfumo dume kutawala hali ambayo inachangia kuongezeka kwa vifo vya wakinamama utokana wazazi wa kiume kutowajali wake kwa mambo ya msingi yanayosaidia uzazi salama.

Maendaenda alisema kuwa hali hiyo ndio ilichangia mkoa wa Rukwa awali kuwa na idadi kubwa ya vifo vya wajawazito, lakini kutokana na jitihada mbalimbali ikiwemo mradi wa TEMP kutoa elimu ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi, wengi wametambua wajibu wao wa kushiriki katika suala zima uzazi kwa wake zao hususani kipindi chote cha ujauzito, kujifumngua na malezi ya familia hivyo imesaidia kupunguza vifo hivuo.

Aliongeza kuwa RFSU inajipanga kuelekeza nguvu zake kwenye mikoa ya Tabora na Katavi ambayo nayo ina idadi kubwa ya vifo vya wajawazito ili kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuachana na mfumo dume ambayo ni chachu ya ongezeko la vifo.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa TEMP mkoa wa Rukwa, Dk John Komba alisema kuwa elimu ya afya ya uzazi imesaidia sana kupunguza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na  ushiriki wa  wanaume katika la yote ya uzazi umekuwa mkubwa kwani wengi  wamekuwa na mwamko wa kuwasindikiza wake zao kliniki kabla na baada ya kujifungua.

Dk. Komba alisema kwamba mathalani vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika hususani Kata ya kirando na Wampembe, ambapo asilimia 75 ya wanaume wamekuwa wakiwasindikiza wake zao na watoto kliniki.

"siku za nyuma wanaume walikuwa hawataki kusikia habari ya kumsindikiza mwanamke kliniki lakini baada ya elimu hii mabadiliko ni makubwa sana hasa katika maeneo ya mwambao wa ziwa Tanganyika" alisema mratibu huyo wa TMEP
.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa