Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Walter mguluchuma
Sumbawanga.
UONGOZI wa Halmashauri
ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo
mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza
darasa la saba wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
Kaimu Mkurugenzi wa hamashauri hiyo, Matrida Mwinuka alisema hayo
wakati akifungua mafunzo ya stadi za KKK yaliyowashirikisha walimu wa
darasa la kwanza na pili wa shule 37 za wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
yaliyofanyika juzi kwenye ukumbi wa kituo cha walimu TRC kilichopo
katika mji mdogo wa Matai wilayani humo.
Mwinuka alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha
halmashauri hiyo inaondokana na idadi ya wanafunzi wasiojua kusoma,
kuhesabu na kuandika (KKK) ambao mjongoni mwao wamekuwa wakihitimu elimu
ya msingi kila mwaka.
"kimsingi tumejizatiti kuhakikisha tunawapa elimu ya stadi za kkk
walimu wetu wanaofundisha wanafunzi wa darasa la saba ili kuhakikisha
tunakuwa na wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi wakijua kusoma,
kuhesabu na kuandika hiyo ndio njia mojawapo ya kutekeleza mpango wa
matokeo makubwa sasa (BRN) kupitia sekta ya elimu" alisema Mwinuka
ambaye pia Ofisa elimu taaluma shule za msingi kwenye halmashauri hiyo.
Naye ofisa elimu taaluma shule za msingi Christina Bukori alisema
kuwa hivi sasa idadi ya watoto wasiojua KKK waliopo darasa la saba ni
238 hivyo hali hiyo ndio imesababisha kufanyika kwa mafunzo hayo ya
kuwajengea uwezo walimu hao ili waweze kuwafundisha watoto hao na
wengineo na kuondokana kabisa na changamoto hiyo.
Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo, Ezekiel Lipingu alisema
kuwa msingi mibaya ya kuwaandaa walimu katika vyuo husika ndio sababu
ya ongezeko la wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui
kusoma kuhesabu na kuandika.
Alitaka kuwepo kwa utaratibu mzuri wa kuwaanda walimu katika vyuo
hivyo ili watoke hapo wakiwa na stadi za kutosha za kumfanya mwalimu
aweze kujua stadi hizo za kusoma, kuhesabu na kuandika.
Home »
» UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma
UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, umeanza kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuhakikisha wanaondoa kabisa idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment