Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Walter Mguluchuma
Sumbawanga.
JAMII kutofahamu haki za msingi
za afya ya uzazi na mifumo dume ni miongoni mwa sababu zinazochangia
kuongezeka kwa vifo vya wanawake wajawazito katika mikoa ya mbalimbali
hapa nchini, imefahamika.
Meneja Mradi wa shirika la Swedish Association for Sexuality
Education (RFSU) Cuthbert Mendaenda,alisema hayo wakati akizungumza
kwenye kikao wakuu wa vyuo mbalimbali kilicholenga kuwafahamisha kuhusu
mradi wa Tanzanian Men as Equal Partners (TMEP), kilichofanyika jana
kwenye ukumbi wa Libori mjini hapa.
Alisema kuwa utafiti waliofanya wamebaini kuwa wananchi wengi hasa
vijijini hawajui haki za msingi za afya ya uzazi hivyo kuipa mwanya
mfumo dume kutawala hali ambayo inachangia kuongezeka kwa vifo vya
wakinamama utokana wazazi wa kiume kutowajali wake kwa mambo ya msingi
yanayosaidia uzazi salama.
Maendaenda alisema kuwa hali hiyo ndio ilichangia mkoa wa Rukwa
awali kuwa na idadi kubwa ya vifo vya wajawazito, lakini kutokana na
jitihada mbalimbali ikiwemo mradi wa TEMP kutoa elimu ushiriki wa
wanaume katika afya ya uzazi, wengi wametambua wajibu wao wa kushiriki
katika suala zima uzazi kwa wake zao hususani kipindi chote cha
ujauzito, kujifumngua na malezi ya familia hivyo imesaidia kupunguza
vifo hivuo.
Aliongeza kuwa RFSU inajipanga kuelekeza nguvu zake kwenye mikoa ya
Tabora na Katavi ambayo nayo ina idadi kubwa ya vifo vya wajawazito ili
kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuachana na mfumo dume ambayo ni
chachu ya ongezeko la vifo.
Kwa upande wake, Mratibu wa mradi wa TEMP mkoa wa Rukwa, Dk John Komba
alisema kuwa elimu ya afya ya uzazi imesaidia sana kupunguza matukio ya
unyanyasaji wa kijinsia na ushiriki wa wanaume katika la yote ya uzazi
umekuwa mkubwa kwani wengi wamekuwa na mwamko wa kuwasindikiza wake zao
kliniki kabla na baada ya kujifungua.
Dk. Komba alisema kwamba mathalani vijiji vya mwambao wa ziwa
Tanganyika hususani Kata ya kirando na Wampembe, ambapo asilimia 75 ya
wanaume wamekuwa wakiwasindikiza wake zao na watoto kliniki.
"siku za nyuma wanaume walikuwa hawataki kusikia habari ya kumsindikiza
mwanamke kliniki lakini baada ya elimu hii mabadiliko ni makubwa sana
hasa katika maeneo ya mwambao wa ziwa Tanganyika" alisema mratibu huyo
wa TMEP.
Home »
» Elimu ya afya ya uzazi chachu ya kupunguza vifo vya wajawazito.
Elimu ya afya ya uzazi chachu ya kupunguza vifo vya wajawazito.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment