WANACCM RUKWA WAASWA KUTOKUMBATIA UDINI NA UKABILA.

 Mbunge wa Nkasi Kasikazini Desderius Mipata akichangia mada katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika jana kwenye ukumbi mikutano wa mkoa huo (RDC) picha na Mussa Mwangoka.
 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa jumuiya ya vijana ya CCM Sumbawanga mjini wakifuatilia kwa makini maelekezo waliyokuwa wakipewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.

 Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Sumbawanga mjini, John Myovela akizungumza jana wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa umoja huo uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
Mbunge wa Nkasi Kusini, Ali Keisy akichangia mada katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika jana kwenye ukumbi mikutano wa mkoa huo (RDC) picha na Mussa Mwangoka.
----------------------

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa wametahadharishwa kuachana na siasa za udini na ukabila kwa kuwa athari zake ni kuligawa taifa na kuhatarisha amani iliyopo.

Katibu wa uchumi na fedha wa CCM mkoa huo, Anyosisye Kiluswa alisema jana wakati wakifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Sumbawanga mjini uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa.

Alisema kuwa siasa za udini na ukabila hazipaswi kupewa nafasi ndani ya Chama hicho tawala ambacho baadhi ya jumuiya zake zimeanza kuchagua viongozi wake, kwani athari za udini ni kubwa kwa siku za usoni ambapo zikikomaa zitaligawa taifa na hatimaye kuhatarisha amani iliyopo nchini.

" Sisi viongozi hatupaswi kukaa kimya tunapoona siasa chafu za udini na ukabila zinaanza kupenyezwa katika chaguzi za CCM..... ni jukumu letu kukemea na nawaeleza vijana msikubali kuyumbishwa na kuchagua watu wa kufuata misingi isiyo sahihi, ambayo hata hayati baba wa taifa alikemea sana" alisema Kiluswa.

Kiluswa ambaye amechukua fomu ya kugombea wa nafasi ujumbe wa Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (Nec) Sumbawanga mjini, pia alikemea tabia ya baadhi ya wanaccm ambao wana uchu wa madaraka ambao wamekuwa wepesi kukihama chama hicho mara baada ya kukosa nafasi za uongozi wanazotaka. 

Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Sumbawanga mjini, John Myovela aliwataka vijana kutotumika ovyo kwa maslahi ya watu wachache ambao wamekuwa wakitoa rushwa hasa nyakati za uchaguzi na badala yake waweke mbele maslahi ya chama.

Katika mkutano huo wa uchaguzi huo, Velonica Kilala alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Uvccm Sumbawanga mjini, ambapo nafasi za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa zilikwenda kwa Daniel Thomas na Michael Chang'a.


UFISADI RUKWA! WAKURUGENZI WAKOPESHANA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO

 Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa (RCC) leo mjini Sumbawanga. PIcha zote na Mussa Mwangoka.
 Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Desderius Mipata akiwa na Mbunge wa Kwela Ignas Malocha wakifuatilia kwa makini kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa (RCC) kilichofanyika leo mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushauri wa mkoa wa Rukwa (RCC) wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika leo mjini Sumbawanga, picha na Mussa Mwangoka.
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu
 ------------------------------------------------

Mussa Mwangoka,Sumbawanga-Rukwa Yetu

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya amekema  tabia ya baadhi ya  Wakurugenzi wa halmashauri  za Wilaya , Miji na Manispaa mkoani Rukwa  kujikopesha  fedha za miradi ya maendeleo .

Akizungumza  katika Kikao cha  Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Rukwa (RCC) jana  Mkuu huyo wa Mkoa  alisema  kuwa kumeibuka tabia  kwa baadhi ya  Halmashauri  kujikopesha fedha  za miradi  ya maendeleo  hivyo kusababisha  kuwa na miradi  ambayo ni  viporo .

Mhandisi Manyanya alisema kuwa Halmashauri  ziache mara moja kuibua miradi mipya ya maendeleo  kabla ya kuhakikisha viporo vyote vinamalizika  na zifanya jitihada kurudisha  fedha hizo  za miradi  mara moja.

Alisema kuwa  imebainika kwamba  mchezo huo mchafu  umekuwa ukifanyika kutokana  na  Halmashauri  kutofanya  vikao  ambavyo vipo kwa mujibu kwa sheria   tabia  ambayo  nayo inapaswa  iachwe mara moja  kwani imekuwa ikisababisha kupatikana kwa  hati chafu  na kushusha mapato ya halmashauri  sambamba na ufanisi  kwa  watumishi wake .

Katika hatua  nyingine  alisema ili kuepuka  na uhitaji mkubwa wa ardhi  ni vema  makampuni yaliyoonesha nia ya kuwekeza  katika kilimo  kushirikiana na wakulima  kwa maeneo  ambayo  yanaweza kustawisha mazao  wanayoyalenga ambayo  ni  shayiri  na ngano.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kuto washirikisha wananchi  imekuwa ni  changamoto  ambazo  wakati mwingine inakwamisha  uwekezaji  kitu ambacho  sio sahihi  hivyo  mkoa umeliona hilo  na unalazimika sasa kuwa  na mipango  mahususiwa matumizi  bora ya ardhi.

Hata hivyo  siku  za karibuni  makampuni makubwa ya kibiashara  ya Azam- Bakharesa na Kampuni ya kutengeneza Bia nchini (TBL) yameonesha nia  ya kuwekeza  katika kilimo  cha ngano  na shayiri kupitia wakulima wadogo na wale wa kati.
Blogzamikoa 

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA UONGOZI WA TBL UNAOTAKA KUWEKEZA KWENYE ZAO LA SHAIRI MKOANI RUKWA



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL) uliomtembelea ofisini kwake leo ukiwa na lengo la kuwekeza kwenye kilimo cha shairi ambayo ni malighafi muhimu katika kiwanda hicho cha kutengeneza bia nchini. Mkoa wa Rukwa una ardhi yenye rutuba kustawisha mazao mbalimbali ya kilimo ikiwemo mchele, mahindi, maharagwe, ngano, alizeti, mtama, ulezi n.k. Katika kuwekeza kwao wataanza kwa kushirikiana na wakulima wadogowadogo ambao wapo Mkoani Rukwa kwa kuwawezesha zana bora za kilimo hicho pamoja na pembejeo ambapo pia watamiliki mashamba yao wenyewe kwa ajili ya kilimo hicho.

Ndugu Gerry Van Den Houten ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazaji wa Sabmiller ya South Africa ambayo ina mashirikiano na TBL akielezea lengo na faida za uwekezaji huo ambao licha faida kubwa itakayopatikana pia itatoa ajira kwa vijana wengi Mkoani Rukwa pamoja na kuhamasisha kilimo cha zao hilo. Kulia kwake ni Bennie Basson ambaye ni Menenja wa Shairi wa kiwanda hicho cha bia cha Tanzania (TBL).

Timu ya Uongozi wa TBL ambayo pia ilikuwa imeongozana na baadhi ya wakulima wadogowadogo wa shairi Mkoani Rukwa wakiwa Ofsini kwa Mkuu wa Mkoa huo kwenye mazungumzo juu ya uwekezaji huo.
Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, baadhi ya viongozi wa Mkoa na Viongozi wa TBL uliombatana na baadhi ya wakulima wadogowadogo wa shairi Mkoani Rukwa. 
(Picha na Hamza Temba-Rukwareviw blog-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

TANESCO YAAHIDI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA UMEME SOKO LA SAMAKI LA KASANGA


Soko la Samaki la
Kasanga.
 Mazungumzo yakiendelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa
Emmanuel Kachewa, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, Mrs.
Katyega, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO
Maneno Katyega, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Katibu Tawala
Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo
Florence Mtepa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa
Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega Ofsini kwake jana alipotembelea
Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo
alitembelea Soko la Samaki la Kasanga pamoja na kujionea maendeleo ya mradi wa
umeme kwenda Wilaya ya Nkasi.

Hakika ziara ya
Mkurugenzi huyo Msaidizi imekuwa ya mafanikio makubwa kwani baada ya kutembelea
Soko kubwa la Samaki la Kasanga na kujionea umuhimu uliopo wa nishati ya umeme
katika kuendesaha soko hilo ameahidi kupitia Shirika lake kuwa soko hilo
litapatiwa Jenereta kubwa mbili kila moja ikiwa na uwezo wa 50KV. Alisema kuwa
Umeme utakaozalishwa kutokana na Jenereta hizo utaweza pia kuhudumia Vijiji vya
jirani vinavyolizunguka Soko hilo.
Jitihada za kulipatia Soko hilo umeme
zimekuwa zikipewa msukumo mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya ambae amekuwa akilifuatilia kwa karibu ambapo amefanikiwa kumpeleka
kiongozi huyo wa Tanesco hadi eneo la mradi huo ikiwa ni katika jitihada zake za
kutekeleza agizo la Mhe. Makamu wa Rais alipofanya ziara yake Mkoani Rukwa na
kutoa agizo kwa uongozi wa Mkoa ushirikiane na Tanesco kuhakikisha Soko hilo
linapatiwa umeme.
Akiwa Mkoani hapa Kiongozi huyo wa Tanesco alikuta
baadhi ya mapungufu katika utekelezaji wa mradi utakaopeleka umeme Wilayani
Nkasi ambapo walishauriana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambapo walikubaliana
litafutwe suluhu la changamoto hizo badala ya kulaumiana ili kukamilisha mradi
huo muhimu kwa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa
ujumla.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi
Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega (Kushoto) na Kaimu
Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa walipotembelea
Soko la Samaki la Kasanga jana.Picha na Habari na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa-Hamza Temba


 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa