Home » » WANACCM RUKWA WAASWA KUTOKUMBATIA UDINI NA UKABILA.

WANACCM RUKWA WAASWA KUTOKUMBATIA UDINI NA UKABILA.

 Mbunge wa Nkasi Kasikazini Desderius Mipata akichangia mada katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika jana kwenye ukumbi mikutano wa mkoa huo (RDC) picha na Mussa Mwangoka.
 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa jumuiya ya vijana ya CCM Sumbawanga mjini wakifuatilia kwa makini maelekezo waliyokuwa wakipewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.

 Aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Sumbawanga mjini, John Myovela akizungumza jana wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa umoja huo uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
Mbunge wa Nkasi Kusini, Ali Keisy akichangia mada katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Rukwa kilichofanyika jana kwenye ukumbi mikutano wa mkoa huo (RDC) picha na Mussa Mwangoka.
----------------------

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Rukwa wametahadharishwa kuachana na siasa za udini na ukabila kwa kuwa athari zake ni kuligawa taifa na kuhatarisha amani iliyopo.

Katibu wa uchumi na fedha wa CCM mkoa huo, Anyosisye Kiluswa alisema jana wakati wakifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Sumbawanga mjini uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa.

Alisema kuwa siasa za udini na ukabila hazipaswi kupewa nafasi ndani ya Chama hicho tawala ambacho baadhi ya jumuiya zake zimeanza kuchagua viongozi wake, kwani athari za udini ni kubwa kwa siku za usoni ambapo zikikomaa zitaligawa taifa na hatimaye kuhatarisha amani iliyopo nchini.

" Sisi viongozi hatupaswi kukaa kimya tunapoona siasa chafu za udini na ukabila zinaanza kupenyezwa katika chaguzi za CCM..... ni jukumu letu kukemea na nawaeleza vijana msikubali kuyumbishwa na kuchagua watu wa kufuata misingi isiyo sahihi, ambayo hata hayati baba wa taifa alikemea sana" alisema Kiluswa.

Kiluswa ambaye amechukua fomu ya kugombea wa nafasi ujumbe wa Halmashauri kuu ya taifa ya CCM (Nec) Sumbawanga mjini, pia alikemea tabia ya baadhi ya wanaccm ambao wana uchu wa madaraka ambao wamekuwa wepesi kukihama chama hicho mara baada ya kukosa nafasi za uongozi wanazotaka. 

Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Sumbawanga mjini, John Myovela aliwataka vijana kutotumika ovyo kwa maslahi ya watu wachache ambao wamekuwa wakitoa rushwa hasa nyakati za uchaguzi na badala yake waweke mbele maslahi ya chama.

Katika mkutano huo wa uchaguzi huo, Velonica Kilala alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Uvccm Sumbawanga mjini, ambapo nafasi za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa zilikwenda kwa Daniel Thomas na Michael Chang'a.


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa