Home » » UFISADI RUKWA! WAKURUGENZI WAKOPESHANA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO

UFISADI RUKWA! WAKURUGENZI WAKOPESHANA PESA ZA MIRADI YA MAENDELEO

 Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa (RCC) leo mjini Sumbawanga. PIcha zote na Mussa Mwangoka.
 Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Desderius Mipata akiwa na Mbunge wa Kwela Ignas Malocha wakifuatilia kwa makini kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Rukwa (RCC) kilichofanyika leo mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.
 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushauri wa mkoa wa Rukwa (RCC) wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika leo mjini Sumbawanga, picha na Mussa Mwangoka.
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu
 ------------------------------------------------

Mussa Mwangoka,Sumbawanga-Rukwa Yetu

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya amekema  tabia ya baadhi ya  Wakurugenzi wa halmashauri  za Wilaya , Miji na Manispaa mkoani Rukwa  kujikopesha  fedha za miradi ya maendeleo .

Akizungumza  katika Kikao cha  Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Rukwa (RCC) jana  Mkuu huyo wa Mkoa  alisema  kuwa kumeibuka tabia  kwa baadhi ya  Halmashauri  kujikopesha fedha  za miradi  ya maendeleo  hivyo kusababisha  kuwa na miradi  ambayo ni  viporo .

Mhandisi Manyanya alisema kuwa Halmashauri  ziache mara moja kuibua miradi mipya ya maendeleo  kabla ya kuhakikisha viporo vyote vinamalizika  na zifanya jitihada kurudisha  fedha hizo  za miradi  mara moja.

Alisema kuwa  imebainika kwamba  mchezo huo mchafu  umekuwa ukifanyika kutokana  na  Halmashauri  kutofanya  vikao  ambavyo vipo kwa mujibu kwa sheria   tabia  ambayo  nayo inapaswa  iachwe mara moja  kwani imekuwa ikisababisha kupatikana kwa  hati chafu  na kushusha mapato ya halmashauri  sambamba na ufanisi  kwa  watumishi wake .

Katika hatua  nyingine  alisema ili kuepuka  na uhitaji mkubwa wa ardhi  ni vema  makampuni yaliyoonesha nia ya kuwekeza  katika kilimo  kushirikiana na wakulima  kwa maeneo  ambayo  yanaweza kustawisha mazao  wanayoyalenga ambayo  ni  shayiri  na ngano.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kuto washirikisha wananchi  imekuwa ni  changamoto  ambazo  wakati mwingine inakwamisha  uwekezaji  kitu ambacho  sio sahihi  hivyo  mkoa umeliona hilo  na unalazimika sasa kuwa  na mipango  mahususiwa matumizi  bora ya ardhi.

Hata hivyo  siku  za karibuni  makampuni makubwa ya kibiashara  ya Azam- Bakharesa na Kampuni ya kutengeneza Bia nchini (TBL) yameonesha nia  ya kuwekeza  katika kilimo  cha ngano  na shayiri kupitia wakulima wadogo na wale wa kati.
Blogzamikoa 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa