Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RC Rukwa (kushoto aliyevaa miwani) akipokea maelekezo kutoka katika moja ya mabanda ya SAGCOT
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa KamishnMstaafu Zelote Stephen ameishauri kamati ya
maandalizi ya nanenane nyanda za juu kusini kufikiria kushirikisha nchi
za SADC ili kuongeza hamasa na kuleta ushindani kwa watanzania wafahamu
yanayofanyika katika nchi za jirani.
Ametoa
ushauri alipokuwa akifanya majumuisho baada ya kutembelea mabanda 16 ya
bidhaa mbalimbali za kilimo katika maonesho ya nane nane kwa kanda ya
nyanda za juu kusini yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale
jijini Mbeya ambapo Mh. Zelote Stephen alikuwa mgeni rasmi wa siku ya
tatu tangu ufunguzi wa maonesho hayo.
“Tuachane
na mazoea, maonyesho haya yana miaka 25 sasa tuyaboreshe zaidi, isiswe
ni mikoa hii tu saba, tupanue wigo, kwakiwa huku ni nyanda za juu kusini
basi tufikirie kuzishirikisha nchi za SADC ambazo zitasaidia
kubadilishana biashara na teknolojia pamoja na kutafuta masoko,”
Alifafanua.
Akisisitiza
suala hilo Mh. Zelote alibainisha kuwa nchi ya Tanzania inafikika kwa
njia zote, ardhini, majini na angani huku akitaja meli mbili
zilizozinduliwa Mkoani Mbeya na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa, treni ya
TAZARA pamoja na ndege zinazomilikiwa na nchi yetu.
Aidha
amezishauri halmashauri kuanza maandalizi kwa kuwa na siku maalum
kwaajili ya maadhimisho hayo kihalmashauri ili kuwapa ujuzi na kujua
ubora wa vitu ambavyo vinaweza kupelekwa kwenye maadhimisho ya nanenane
kikanda ili kuimarisha ushindani na kumpa kila mwananchi nafasi ya
kuelimika ili kuwa na kilimo chenye tija.
Akiunga
Mkono Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kilolo Ntila alityekuwemo katika msafara huo
alisisitiza kuwa maonesho ya nanenane yanayofanyika kikanda yanalenga
watu wenye kipato cha kutoka katika halmashauri zao na kukusanyika
jijini Mbeya huku wakulima wasio na uwezo wakikosa elimu inayopatikana
kutokana na maonyesho hayo.
“Nikiongezea
aliyoyasema Mheshimiwa Mkuu wangu wa Mkoa, kwa nafasi yake namuomba
aweze kushawishi haya makampuni makubwa kuweza kusambaza wataalamu wao
katika Halmashauri zetu ambapo kuna uhitaji mkubwa wa elimu hii
inayotolewa hapa katika viwanja hivi vya nanenane na wao ndio walengwa
wakubwa wa shughuli hii,” alisema.
Pamoja
na hayo Mh. Zelote alitoa wito kwa wananchi wote wenye nafasi
wajitokeze kwa wingi kwenye maonyesho hayo ili waweze kuelimika kutokana
na mafunzo mbalimbali yanayotolewa viwanja hivyo vya nanenane na kusifu
maandalizi ya sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment