Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma .
Rukwa yetu Blog
Mahakama kuu ya Sumbawanga imewahukumu watu wawili Kunyongwa hadi kufa katika kesi mbili tofauti baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kusudia wake zao huku mmoja akipatikana na hatia ya kumuua mke wake mkubwa baada ya kumtuhumu kumuua kwa ushirikina mke wake mkubwa kuwa amemuaua mtoto wake wa mke wake mdogo .
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Jaji wa Mahakama kuu ya Sumbawanga Jaji Adamu Mambi katika kikao cha Mahakama kuu ya Sumbawanga kilichofanyika katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi .
Katika kesi ya kwanza Mahakama kuu ilimuhukumu Shija Sosoma Mkazi wa Kijiji cha Mamba Wilaya ya Mlele kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kusudia mke wake mkubwa kwa kumchinja baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi kuwa alimuua mtoto wake wa mke wake mdogo kwa ushirikina .
Awali kwenye kesi hiyo mwendesha mashitaka mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi Achiles Mulisi alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo hapo Januari 23 mwaka 2012 huko katika Kijiji cha Mamba .
Ilidaiwa kuwa siku hiyo hiyo mshitakiwa Shija Sosomo alimchinja mke wake mkubwa aitwaye Mwashi Nkuba baada ya kumshutumu kuwa amemuua kichawi mtoto wake wa mke mdogo .
Mwendesha mashita huyo alidai kuwa mshitakiwa baada ya kufanya mauwaji hayo alikwenda kutowa taarifa kwa balozi wa nyumba kumi na kumweleza kuwa amafanya mauwaji ya kumuua mke wake mkubwa kwa kuwa amemuua mtoto wake wa mke mdogo .
Katika kesi hiyo mshitakiwa alikuwa akitetewa na mwanasheria Elias Kifunda ambapo upande huo haukuwa na shahidi yoyote zaidi ya mshitakiwa mwenyewe huku upande wa mashitaka ukiwa na mashihidi sita .
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adamu Mambi aliiambia Mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo Mahakama pasipo shaka yoyote imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashita hivyo mshitakiwa amepatikana na hatia ya kifungu cha sheria namba 196 na 197 kuua kwa kusudia
Hivyo alitowa nafasi kwa mshitakiwa ya kujitetea kabla haja somewa hukumu hata hivyo wakili Elias Kifunda aiieleza Mahakama kwa kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia hiyo ambayo adhabu yake ni moja tuu kwa hiyo Mahakama itowe hukumu kwa jinsi sheria inavyoelekeza .
Nae Mwanassheria wa Serikali Achiles Mulisi aliiomba mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa kwani mauwaji ya kuuawa kwa wanake yameshamiri sana mkoani Katavi hivyo adhabu kali ikitolewa kwa mshitakiwa huyo itakuwa ni funzo kwa watu wengine.
Jaji Adamu baada ya kusikiliza utetezi huo alisoma hukumu na kueleza kuwa mshitakiwa mahakama imemuhukumu mshitakiwa kwa kosa la kifungo cha sheria Namba 26 ambapo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa .
Katika kesi nyingine Mahakama kuu ya Sumbawanga imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Monde Ndushi 52 Mkazi wa Kijiji cha Chamalendi Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake kwa makusudi .
Mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali Jamila Mziray aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Machi 12 mwaka 2016.
Siku hiyo ya tukio mshitakiwa alidaiwa kumuuwa mke wake aitwaye Ngole Njile kwa kumchoma na visu baada ya kukasirishwa na kitendo cha marehemu kumnyima mahindi ndugu yake .
Mshitakiwa katika kesi hiyo alitetewa na wakili Elias Kifunda ambapo katika utetezi wake alidai kuwa yeye hakutenda kosa hilo na siku hiyo ya tukio hakuwepo nyumbani kwake bali alikuwa amesafiri .
Baada ya kusikliza pande hizo mbili Jaji Adamu Mambi alitowa nafasi kwa upande wa utetezi kuweza kujitetea kabla ya kusomwa kwa hukumu ambapo wakili Elias aliiomba Mahakama itowe adhabu kwa mujibu wa sheria inavyo eleza kwani kosa hilo adhabu yake ni moja .
Mwanasheria wa Serikali Jamila Mziray aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa kwani kitendo alichokifanya ni cha kikatili na pia amewasababishia watoto wa marehemu kukosa huduma za mama yao ambazo walikuwa bado wanazihitaji .
Akisoma hukumu hiyo Jaji Adamu Mambi aliiambia Mahakama kuwa mshitakiwa amepatikana na hatia ya kosa la kifungu cha sheria namba 196 na 197 hivyo mahakama imemuhukumu Monde Ndusha kunyongwa hadi kufa .
0 comments:
Post a Comment