Home » » NAIBU WAZIRI WA ELIMU AAGIZA WALEMAVU WAJENGEWE VYOO VYAO

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AAGIZA WALEMAVU WAJENGEWE VYOO VYAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



NAIBU Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amemuagiza msimamizi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Kantalamba kuhakikisha kuwa walemavu wanajengewa vyoo vyao ndani ya mabweni wanamolalia nia ikiwa ni kujiepusha na kuwaamsha wenzao usiku pindi wanapotaka kwenda chooni.Ametoa agizo hilo leo jumapili (30/7/2017) muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule hiyo iliyopo Wilayani Sumbawanga iliyopewa Shilingi Bilioni 1.1 ikiwa ni mpango wa serikali wa kuzirudishia hadhi shule kongwe nchini huku shule hiyo ikiwa ni ya tangu 1964.

“Lazima muhakikishe kwamba Mnakuwa na vyumba maalum kwaajili ya wanafunzi wenye ulemavu na kuwawekea miundombinu hasa kwa wale walemavu ambao mazingira yao ni magumu Zaidi, kwa mfano mwanafunzi ana ulemavu wa miguu na anatakiwa kwenda chooni hapaswi kutambaa kwenye mikojo ya wanafunzi wenziwe hii inawapelea wao kuwa katika mazingira hatarishi zaidi,” Alisema.

Mbali na agizo hilo pia Mhandisi Manyanya ametoa wiki tatu ukarabati wa shule hiyo kumalizika baaada ya muda waliopangiwa kumalizika huku kipaumebele kikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.

“Sijaridhishwa na kasi ya ukarabati huu hivyo tumewaongezea wiki tatu mhakikishe mnamaliza ili wanafunzi waendelee na masomo maana yake kama mngekuwa hamwezi kumaliza kwa wakati kwanini msingesema mapema,” Alisisitiza.

Aidha alipokuwa anakagua bwalo la kulia wanafunzi aliagiza kutanuliwa kwa bwalo hilo baada ya kuona kuwa bwalo hilo ni dogo na wanafunzi ni wengi kiasi ambacho ingewabidi wanafunzi hao kula kwa zamu ili wote waweze kulitumia bwalo hilo na kuongeza kuwa ukarabati unaofanyika ni pamoja na utanuzi wa majengo kwani ukubwa wa jengo lililopo ni wa tangu 1964 na sasa ni 2017.

Kabla ya kumaliza ziara yake shuleni hapo aliwasisitizia wanafunzi kuwa nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa hakuna tofauti kati ya shule za serikali na shule binafsi kuanzia huduma za majengo, elimu na vifaa vya kusomea.



Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa