Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemuagiza afisa afya
wa wilaya ya Kalambo kuhakikisha anakagua usafi wa vyoo na maeneo yanayo
zunguka nyumba kwa wilaya nzima ili kujiepusha na ugonjwa wa
Kipindupindu katika Wilaya hiyo.
Ametoa
agizo hilo katika mkutano na wananchi siku ya usafi wa mwisho wa mwezi
maarufu kama “Magufuli Day” baada ya Mkuu huyo kukagua nyumba 12, maduka
ya wafanyabiashara pamoja na soko katika makao makuu ya wilaya hiyo
huku nia ikiwa ni kutaka kujua hali ilivyo wanakojisaidia, wanakohifadhi
taka pamoja na hali ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Katika
ukaguzi huo amebaini kuwa wananchi wengi husafisha nje ya nyumba tu
huku nyuma ya majumba yao hali ikiwa mbaya jambo ambalo hupelekea
kuibuka kwa kipindupindu na kuisababishia serikali kuwa katika wakati
mgumu kwa magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika endapo usafi utazingatiwa.
“Leo
nilipenda nione usafi wa matai, nimeuona na nimetoa “marks” 60,
Nimepita karibu maeneo mbali mbali, usafi mnaoufanya ni wakuficha uchadu
kidogo, huku mbele kusafi lakini nyuma kuchafu sana, nawaomba hilo
mlirekebishe” Alisema.
Pia
aliishauri halmashauri hiyo ya kalambo kuweza kusimamia sharia za usafi
zilizopo bila ya huruma ili kuleta mabadiliko na kuitaka halmashauri
hiyo kutenga fedha za makusanyo ya ushuru ili kuweza kuboresha hali ya
usafi katika mji huo.
Mwezi
mmoja uliopita Wilaya hiyo ilikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu na kuua
mtu mmoja na kuwaacha wengine ishirini katika hali mbaya jambo ambalo
serikali haitaki ijirudie.
“Juzi
hapa kulitokea kipindupindu kule Kijiji cha Samazi, hapana hatutaki
watu wafe kwa kipindupindu, sasa nimeona choo kinamwaga maji machafu
kinyesi kinatoka nje bata wanapokea wanakula, hatupo salama,”
Alimalizia.
Pamoja
na hayo Mh. Zelote alisisita kuwa usafi ni wa kila siku si lazima
kusubiri jumamosi ya mwisho wa mwezi na kueleza kuwa siku hiyo imewekwa
maalum ili kuwakumbusha wananchi kuwa wanahitajika kufanya usafi maeneo
wanayofanyia biashara pia na kuwa usafi ni muhimu.
0 comments:
Post a Comment