Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda, Matini Kapufi (42 ) na
Katekista wa kanisa hilo wa kijiji cha Mtakuja, Parokia ya Inyonga,
Patrick Mwendowasaa (60), wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa
wakisafiria kupinduka.
Gari hilo lilipinduka baada ya kuacha njia. Watu wengine wawili walijeruhiwa na wamelazwa hospitali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri
Kidavashari alisema ajali hiyo ilitokea jana saa nne asubuhi katika
Kijiji cha Kamsisi, Tarafa ya Inyonga, Barabara ya Inyonga kuelekea
mkoani Tabora.
Alisema ajali hiyo ililihusisha gari aina ya
Toyota Hilux, Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Padri Kapufi ambaye ni
Paroko wa Parokia ya Mwese, Jimbo Katoliki la Mpanda.
Aliwataja watu waliojeruhiwa kuwa ni Katekista
Msaidizi wa Kijiji cha Mtakuja, Parokia ya Inyonga, Daud Saveli (31),
ambaye ameumia sehemu za kidevu na mguu wa kushoto na mkazi wa Kijiji
cha Mtakuja, Tarafa ya Inyonga, Wilaya ya Mlele, Melikio Maraluma.
Alisema watu hao walipata ajali walipokuwa
wakisafiri kutoka Inyonga, Makao Makuu ya Wilaya ya Mlele kwenda Mto
Koga, mpakani mwa Mkoa wa Katavi na Tabora kumpokea Askofu Gervas
Nyaisonga aliyekuwa akitokea Dodoma baada ya kuhamishiwa Jimbo la
Mpanda.
Kamanda Kidavashari alisema baada ya gari hilo
kufika Kijiji cha Kamsisi, liliacha njia na kupinduka na kusababisha
kifo cha Katekista Mwendowasaa papohapo na Padri Kapufi aliyefariki
njiani alipokuwa akipelekwa Kituo cha Afya Inyonga.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment