Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifungua rasmi mkutano
wa wadau wa uhamasishaji wa ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP
- ("Public and Private Partnership") katika Sekta ya Afya
uliofanyika leo katika ukumbi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa. Katika hotuba
yake ya ufunguzi amesema ili kufikia lengo kuu la millennia ifikapo mwaka 2015
la kupunguza vifo vya watoto, akina mama wajawazito na kuweza kudhibiti
magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza pamoja na kuboresha mazingira na
kupata maji salama Serikali peke yake haitaweza bila kushirikiana na Sekta
Binafsi ambayo pia imekua na mchango mkubwa katika kujenga afya za watanzani.
Ndugu Paul Michael Nadrie muwezeshaji wa ubia kati ya Sekta
ya Umma na Sekta Binafsi PPP - (Public and Private Partnership) katika
Sekta ya Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwasilisha moja ya
mada katika Mkutano huo. Alieleza kuwa zipo faida nyingi za PPP ikiwemo
kuongeza na kusogeza huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuongeza ushindani
katika kutoa huduma za afya nchini. Akigusia changamoto amesema zipo changamoto
nyingi ikiwemo uelewa hafifu wa PPP kwa watekelezaji na jamii kwa ujumla, uwazi
katika utekelezaji wa PPP (Public and Private Partnership), upatikanaji wa
mikopo ya mda mrefu, uwezo hafifu wa kufanya upembuzi yakinifu na uwezo hafifu
wa kiuchumi katika kushiriki kwenye miradi ya PPP (Public and Private
Partnership).
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akitambulisha wajumbe katika
kikao hicho kutoka Sekta Binafsi na Sekta ya Umma. Kulia ni Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies
Pangisa.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Post a Comment