Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADHI ya watoto wilayani Nkasi, Rukwa hasa maeneo ya vijijini,
wamekuwa wakiajiriwa na familia za wafugaji kwa ujira wa ndama mmoja
kwa mwaka.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini watoto hao
ambao wengi wao ni wa kabila la Wafipa, wamekuwa wakitumikishwa kazi
ya kuchunga ng’ombe na wafugaji wa kabila la Kisukuma.
Mbaya zaidi baadhi ya watoto hao huamua kuacha kabisa masomo na
kwenda kufanya kazi hiyo, ambayo mkataba wake huwa ni malipo ya ndama
yanayofanywa kati ya familia ya mtoto na mfugaji.
Uchunguzi huo pia umebaini baadhi ya watoto kupata vipigo kutoka kwa
wafugaji hao, hasa pale wanapopoteza mifugo wakiwa kazini.
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Lunyala, nje kidogo ya Mji wa Namanyere
wilayani Nkasi, alisema baadhi ya wazazi wanalazimika kuwaingiza
watoto wao katika ajira hizo kutokana na ugumu wa maisha.
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Oscar
Mdenye, alikiri uwepo wa ajira hizo kwa baadhi ya vijiji, jambo ambalo
alisema wanapambana nalo na kuitaka jamii ya maeneo hayo ibadilike na
kuacha ukatili huo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment