Na walter mguluchuma,Sumbawanga
MPANDA baiskeli, Leonard Garimoshi (20), mkazi Kaengesa wilayani Sumbawanga , mkoa wa Rukwa amefariki dunia baada ya kugongwa na gari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda akitihibitisha alibainisha tukio hilo hilo lilitokea kijijini Katonko , Kata ya Kaengesa katika barabara kuu ya Mbeya – Sumbawanga mkoani hapa ajali ya basrabarani iliyohusisha gari aina ya Toyota Raum yenye namaba za usajiri T 186 AYJ lililokuwa likiendeshwa na Soud Hilal .
Kwa mujibu Kamanda Mwaruanda gari hilo lilimgonga mwendesha baiskeli huyo na kufa papo hapo lilikuwa likitokea Sumbawanga mjini likielekea Jijini Dar Es Salaam.
“Chanzo cha ajali hii ya barabarani ni mwendokasi wa dereva wa gari hilo ambaye ameshakamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake “ alibainisha .
Katika tukio lingine Mfanyabishara aitwae Yohana Damian (31) , mkazi wa eneo la Jangwani , Manispaa ya Sumbawanga amevamiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa vibaka akiwa dukani kwake na kuimwibia vitu mbalibali nyenye thamani ya zaidi ya Sh 800,000.
Kamanda Mwaruanda amethibitisha kuwa ‘vibaka’ hao walifanikiwa kutoroka mara tu askari polisi walipofika dukani hapo kwamba jitihada zinaendelea kuwabaini ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment