Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mwendesha Pikiipiki (BODABODA) mmoja anaefanyashughuli zake katika kituo cha Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kiikatili kwa kuchinjwa na kukakatwa na mapanga kisha kupolwa pikipiki yake na mwili wake kutupwa kichani
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishana msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari alimtaja Bodaboda aliyeuwawa kwa kuchinjwa kuwa ni Samweli Joseph Vitalisi (31) Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari tukio hilo la mauwaji ya kusikitisha lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi jioni katika eneo la Kijiji cha Mpembe Kata ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilayani Hapa
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu akiwa kwenye kituo chake cha kufanyia shughuli hapo majira ya saa tisa alasiri akiwa na Bodaboda wenzake alitokea mteja mmoja ambae alimwomba marehemu wafanye nae mazungumzo ya maelewano ya kiwango cha bei ya kumsafirisha kwa kutumia pikipiki yake aina ya SUN LG yenye namba za usajiri T 704 CDQ kwa lengo la kumpeleka katika kijjii cha Mpembe kilichoko umbali wa kilometa 72 kutoka Mjini Mpanda
Alisema katika maongezi yake abiria huyo alimweleza mwendesha pikipi BODABODA kuwa anahitaji usafiri huo iliaweze kwenda kijijini kuchukua fedha kwa ndugu zake kwa ajiri ya kukodi gari la kkusafirishia mweli wa marehemu ndugu yake ambae mwili wake ulikuwaumehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ili aweze kuusafirisha kwenda kwenye Kijiji hicho cha Mpembe kwa ajiri ya mazishi
Kamanda Kidashari alieleza baada ya makubaliano baina yao kati ya Bodaboda na mteja wake walikubaliana kuanza safari ya kwenda kijijini huko licha ya Bodaboda wenzake kumtaka umarehemu awaeleza mahari ambako anampeleka mteja huyo lakini marehemu hakuwa wazi kuwaeleza mahari anakoelekea kwa kuhofia wenzake wanaweza kumshawishi mteja wake achukue bodaboda mwingine
Alisema baada ya marehemu kuondoka hapo juzi hakuweza kuonekana tena kwenye kituo chake cha kazi hadi hapo jana ambapo badaboda wenzake walipopata mashaka ya kutoonekana mwenzao toka alipoondoka na mteja wake na ndipo walipotowa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao waliwasiliana na uongozi wa kijiji hicho juu ya kutoweka kwa marehemu
Kamanda Kidavashari alisema ndipo hapo jana majira ya saa saba mchana mwili wa marehemu ulipookotwa ukiwa kwenye kichaka katika kijiji hicho cha Mpembe huku ukiwa umechinjwa shingo na kukatwa kwa panga kichwani na mkononi na pikipiki yake ikiwa imepolwa
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limetowa wito kwa waendesha pikipiki bodaboda kuacha tabia ya kuwachukua abilia ambao wasio wafahamu na kusafiri nao umbali mrefu hasa kwenye maeneo ya nje ya mjin na jeshi hilo bado linaendelea na msaka wa kuwatafuta na kumtafuta mtu awa watu waliohusika na mauwaji hayo kwani mpaka sasa hakuna mtu alikamaatwa kuhusiana na tukio hilo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment