Mji wa Sumbawanga umekuwa ukipoteza umaridadi wake wa siku za nyuma
kutokana na kuzidi kushamiri kwa ujenzi holela unaofanywa na wakazi wa
mji huo katika siku za karibuni.
Hali hiyo imetajwa kusababishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
kushindwa kugawa viwanja vipya vya ujenzi kwa muda mrefu kutokana na
sababu mbalimbali.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani , Mkurugenzi wa Manispaa
ya Sumbawanga Bw. William Zackaria Shimwela amesema kuwa tatizo la
kutogawiwa kwa viwanja vipya linatokana na Wizara ya Ardhi nyumba na
Makazi kushindwa kupitisha kwa ramani mpya za maeneo ambayo tayari
yamekwishapimwa kwa takribani miaka mitatu sasa, hivyo wananchi kukata
tamaa na kuanza kujengamakazi yao kiholela.
Amesema Manispaa yake hivi sasa haina tatizo la wataalamu na hata vifaa
ambavyo vinatumika kwaajili ya upimaji ambao wako tayari kufanya kazi
muda wote lakini jitihada zao zinakwamishwa na wizara husika.
Awali katika kikao hicho katika maswali ya papo kwa papo , Diwani wa
kata ya Izia, Bw.Field Kasitu aliuliza Mkurugenzi huyo ni lini Manispaa
hiyo itapima maeneo ambayo yamejengwa kiholela ili wananchi waweze
kupata hati za nyumba zao wanazozimiliki.
Katika swali hilo Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa hawawezi kutoa hati
za nyumba kwa wale waliojenga kwenye maeneo yasiyopimwa ilihali akisema
kuwa utaratibu unaendelea kwa baadhi ya maeneo hayo kupitiwa na
wataalamu wa Idara ya ardhi ili yaweze kupimwa na kuchorwa ramani zake.
Home »
» UJENZI HOLELA WASHAMIRI SUMBAWANGA
UJENZI HOLELA WASHAMIRI SUMBAWANGA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment