IMANI za kishirikina zimegubika kijiji cha Iyela,
Kata ya Mkwamba, wilayani Nkasi, Rukwa, na kusababisha walimu sita kati ya 10
wa Shule ya Msingi Mkwamba kukimbia shule hiyo na kuomba wapangiwe shule
nyingine, ili kuokoa maisha yao.
Wakizumgumza na Tanzania Daima kwa niaba ya walimu
wenzao katika shule hiyo, Josephat Kapandila na Jelazi Kakusa, walisema walimu
hao wakiwamo wa kike wamekimbia baada ya kudai kuingiliwa kimwili na wanaume
kwa imani za kishirikina Walisema sakata hilo limedumu kwa muda mrefu sasa na
wametoa taarifa ofisi ya kijiji, ili kupata msaada lakini wamekosa ushirikiano.
Kutokana na hali hiyo, waliiomba Ofisi ya Elimu
Wilaya kuwasaidia na ndipo walimu wawili kati ya wahanga wa tukio hilo
walipopewa uhamisho.
Walisema kuwa walifikiri baada ya walimu hao wa
kike kuondoka shule ingerudi katika utulivu, lakini vitendo hivyo vimeendelea
na walimu wengine kulazimika kuondoka.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Michael Kapela, alisema
licha ya shule hiyo kukumbwa na matatizo hayo ameshangazwa na ofisi ya elimu
wilaya kukubali kuwahamisha walimu bila yeye kujua.
Alisema kawaida kama mwalimu anaomba uhamisho ni
lazima maombi yaanzie kwake, mratibu kata na kisha ngazi ya wilaya, lakini
ofisi ya wilaya imekuwa ikitoa barua za uhamisho bila wao kushirikishwa na
kutaka kujua tatizo hasa ni nini katika shule hiyo kwa lengo la kulitafutia
ufumbuzi.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Ghambi Idon alikiri
kuwapo kwa tatizo kati ya wananchi na walimu wa shule hiyo wakituhumiana walimu
wa kike kuingiliwa kimwili kiushirikina.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment