
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akishiriki kwa vitendo kufyatua matofali na vijana wa CCM
walioweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Mji
mdogo wa laela tarehe 22 Septemba 2013. Lengo
kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera za Chama
cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa ujumla.
Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama
kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha
afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni
Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma akiwahamsisha vijana hao kukipenda
chama chao kwa kuweka uzalendo mbele katika mkutano uliofanyika katika
ofisi za Chama hicho katika mji mdogo wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka
kushoto ni Matin Matete Mjumbe wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli
Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa, Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin
Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Persin Kalikule
Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.

Sehemu ya vijana hao waliotoka katika
maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakionekana
kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo iliyopo katika mji mdogo
wa Laela.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM
Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao akielezea mipango mbalimbali ya
umoja huo ikiwemo uhamasishaji na upandaji miti ya mbao kwa ajili ya
kuwainua vijana kiuchumi Mkoani Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini
ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na viriba
vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM Mkoa wa
Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la upandaji miti
wa kibiashara.
Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
0 comments:
Post a Comment