Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi
akikagua kiwanda cha maji cha Dew Drop kinachomilikiwa na muwekezaji wa
ndani Ndugu Aziz Tawaqal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa tarehe 18 Sept
2013. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Katibu
Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima.
Kiwanda
cha kisasa cha Dew Drop chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa
saa yakiwa na ubora wa hali ya juu. Maji hayo huzalishwa katika hali ya
usafi na hayaongezwi kemikali yeyote ambapo husafishwa kupitia "Sand
Filters", "Activated Coal" na teknolojia ya "UV Light".
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal akitoa maelekezo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William
Lukuvi alipofika kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za
muwekezaji huyo ikiwemo kiwanda cha unga cha Energy Milling.
Waziri
Lukuvi akipokea maelezo ya Maji ya Dew Drop kutoka kwa Mkurugenzi wa
Kampuni ya Vinywaji ya Dew Drop Aziz Tawaqal, Waziri huyo aliyasifia
maji hayo na kusema kuwa ameyanywa na ni mazuri sana ukilinganisha na
maji mengine yanayozalishwa hapa nchini. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
(www.rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment