
Mashine maalum ya kufulia nguo aina ya
HITACHI iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Mizengo Kayanza Pinda kwa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala
Mkoani Rukwa na kukabidhiwa kituoni hapo na Katibu wake wa Jimbo Ndugu
Charles Kanyanda leo tarehe 30, Agosti 2013. Msaada huo wenye thamani ya
Tshs. Milioni moja na nusu (1.5) ni ahadi ya Waziri Mkuu aliyoitoa
alipotembelea kituoni hapo mapema mwaka huu.

Ndudu Charles Kanyanda Katibu wa Jimbo
wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi akimkabidhi Mama Mkuu
Mariastella Wampembe wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni
wamiliki wa kituo cha kulelea mayatima cha Katandala mashine maalum ya
kufulia nguo iliyotolewa na Waziri Mkuu kwa kituo hicho leo tarehe 30,
Agosti 2013.

Mama Mkuu Mariastella Wampembe wa
Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika wamiliki wa kituo cha kulea
mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa akitoa shukrani zake za dhati kwa
Waziri Mkuu kupitia kwa Katibu wake wa Jimbo Ndugu Charles Kanyanda kwa
msaada huo wa mashine ya kufulia.
Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Post a Comment