NA Walter Mguluchuma sumbawanga
Mwamuzi na wachezaji watatu wa timu ya Serengeti SC ya
wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa
wamelazwa kwenye kituo cha Afya cha Laela baada kushambuliwa na kwa kupigwa
sehemu mbalimbali za miili yao katika mchezo wa Ligi ya ujirani mwema.
Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi
Kisalala kata ya Laela Mwamuzi wa mchezo huo Eliaza Simzokwe alishambuliwa dk 75 pale alipovamiwa na kundi la mashabiki
timu ya Serengeti na kumvua nguo zake kisha kuanza kumpiga hadi kujisaidia haja kubwa wakipinga bao lililofungwa
na mchezaji wa timu Muchiza FC, Siyaye Mgonde wakidai alikuwa ameotea kabla ya
kufunga.
Meneja wa Timu ya Serengeti FC ya Kisalala , Andrew William alisema
kuwa baada ya mwamuzi huyo kuvuliwa nguo na kupata kipigo hicho ilibidi baadhi
ya wananchi kuingilia kati na kumwokoa hatimaye mwanamke mmoja alimsaidia kwa
kumfunga khanga ya kumsitili kabla
kukimbizwa kituo cha Afya cha Laela kwa ajili ya matibabu ya majereha mbalimbali
kwenye mwili wake.
Baada ya kuona
Mwamuzi huyo anazidi kushambauliwa ndipo wachezaji na mashabiki wa timu pinzani
ya Muchiza FC waliamua kuingilia kati na kuanza kushambuliana wapinzani wao
hali iliyosababisha wachezaji wawili na kocha watimu ya Serengeti kujeruhiwa na
kulazwa kwenye kituo hicho cha Afya.
Ugomvi huo ambao ulihatarisha maisha ya washabiki na
wachezaji hao ilisababisha kuharibiwa vibaya kwa vyombo vyao vya usafiri ikiwa
ni pamoja na pikipiki na baiskeli 10.
Hatahivyo wakati washabiki wa timu ya Serengeti wakidhani
kuwa ugomvi huo umeishia hapo lakini usiku mashabiki wa timu jirani ya Muchiza
FC kutoka kijiji cha Kitete walikuja tena kuanza kuwasaka wachezaji na washabiki
wa timu ya Serengeti nyumba kwa nyumba na kuwashambulia kwa silaha za jadi
ikiwa ni pamoja na mikuki na mapanga.
Katika ugomvi huo wa usiku huo, mchezaji wa timu ya
Serengeti FC Peter Willy alijeruhiwa kwa kupigwa panga kichwani.
Kufuatia hali hiyo uongozi wa Chama cha soka wilayani
Sumbawanga (SURUFA)kimewatahadharisha washabiki wa mchezo huo kuachana na
vitendo vya vurugu kwenye michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashambulia
waamuzi wa mchezo kwa kuwapiga pale wanapochezesha michezo mbalimbali.
Katibu wa SURUFA, Kanyiki Nsokolo alisema kitendo
kilichofanya na mashabiki hao ni cha kihuni na hakifai kutokea sehemu zingine.
Alisema kufanyika kwa vitendo hivyo ni matokeo ya kuendesha
masuala ya soka kienyeji pasipo kufuata taratibu ikiwa ni pamoja mashindano
hayo kufanywa pasipo kukishirikisha chama cha soka cha wilaya sanjari
kutokuwapo kwa makocha na waamuzi wenye
sifa kwaajili ya kucheza michezo mbalimbali ya soka.
0 comments:
Post a Comment