Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike
wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa
kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja
na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa
maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana
ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa
Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze
kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum
Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi
Catherine Mashalla.
Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo
mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama
hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na
msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji. Mapendekezo mengine
ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka
tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika
kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata
hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni
jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa
kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.
Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika
kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo
rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za
namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na
badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.
Mkuu
wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali
wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na
maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia
mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya
madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary
Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza
kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa www.rukwareview.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment