Na Elizabeth Ntambala wa  www.matukiodaima.com Sumbawanga.

WATU watatu wamefariki dunia katika matukio  tofauti  mkoani Rukwa likiwemo la mmoja kukanyagwa na gari akiwa anampiga ngumi dereva wa gari hilo baada ya kukanyaga dishi alilokuwa akitumia kuoshea viatu.

Kaimu kamanda wa polisi  Longinus Tibishubwamu alisema  katika tukio la kwanza   la kwanza
lilitokea Julai 25 majira ya saa 5 za asubuhi  Wakati Kijana Herman Jackson(30)mkazi wa mjni sumbawanga alipopoteza maisha baada ya kugongwa na gari no T.548 AED Scania  mali ya William Palangyo wa Dar saalam iliyokuwa ikiendeshwa Keneth Mlwilo(29) mkazi wa malangali .

Inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo saa tano asubuhi ya Julai
29 maeneo ya mazwi N.MC.hapa mjini kijana huyo ambaye alikuwa ni mng’alisha
viatu “shoeshiner” alikuwa anaendelea na kazi yake pembeni  ya barabara na ndipo gari hilo lilipompita na
kukata kona ili kuingia mtaaa mwingine ndipo liligonga meza yake ya kufanyia
biashara.

Kaimu Tibishubwana alisema kuwa baada ya kuona hivyo aliamua kulikimbilia na kudandia kwenye mlango wa dereva huku gari  ilikiwa bado  kwenye mwendo kasi akimuashiria dereva asimamishe gari ili wafikie muafaka ,ndipo  Jackson  alidondoka na gari likamkanyaga na kufariki
dunia papo hapo . 


Katika tukio la pili Wiliam Salamba (18) alifariki dunia baada
ya gari alilokuwa amepanda  lenye no
T.296 AMN Toyota Hilux pick up kuacha njia na kugonga gari No T194 BSH Foton
iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa barabara.

Ajali hiyo ilitokea saa 2;30i usiku wa julai 27 maeneo ya
kijiji cha mtimbwa katika barabara ya sumbawanga matai ambapo gari hilo
liliacha njia lilikuwa linaendeshwa na Richard Kana(29)mkazi wa chipu ambaye
alikamatwa na atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi wa awali utakapo
kamilika.

Aidha katika ajali hiyo abiria wanne akiwemo dereva huyo
walipata majeruhi sehemu mbalimbali za miili yao na  uchunguzi unaonyesha ni ulevi wa dereva.

Kaimu Tibishubwana alisema kuwa baada ya kuona hivyo aliamua
kulikimbilia na kudandia kwenye mlango wa dervahuku ilikiwa bado lipo kwenye
mwendo kasi akimuashiria dereva asimamishe gari ili wafikie muafaka ,kwa bahati
mbaya kijna huyo alidongoka na gari likamkanyaga na kufariki dunia papo hapo
.  
 Pia katika  tukio jingine  lililotokea  kijijini Kipa mwambao  mwa Ziwa Rukwa   wilayani Sumbawanga ambapo John mwabulambo(49)  alifariki  dunia  baada ya kushambuliwa  na kundi la
wavuvi  wakimtuhumu  kuiba  nyavu  za kuvulia samaki  yenye  thamani  ya Sh 200,000.

Kwa mujibu wa Tibishubwamu  mtuhumiwa  aitwaye  Andrew Namboti (32)  ananashikiliwa  kwa mahojiano  na Polisi  akihusishwa  na  tukio hilo  kwamba  atafikishwa  mahakamani  mara  tu uchunguzi  wa shauri  lake  hilo  utakapokamilika .
CHANZO MATUKIO DAIMA BLOG