(picha na Lorietha
Laurence-Maelezo)
…………………………………………………………………..
Jennifer Chamila-Maelezo
MKOA
wa Rukwa unatarajia kuanzisha chuo kikuu ambacho kitasaidia vijana
wengi wanaokosa nafasi za kuendelea na elimu ya juu kwa kupata nafasi
ya kujiunga na chuo kikuu.
Mkakati
huo unaosimamiwa na Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa(JUMARU) ambao ni
halali chini ya sheria za nchi ilioanzishwa mwaka 2009 na wakazi wa
mkoa wa Rukwa(Wanarukwa) kwa lengo la kuunganisha nguvu za wanarukwa
wote ili kuleta maendeleo katika mkoa huo na wakazi wake.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa
Sekretariati wa JUMARU Bw.Joachim Sikulumbwe amesema kuwa wameandaa
kongamano la wanarukwa wote waishio jijini Dar es Salaam litakalo
fanyika Septemba 01 mwaka huu,katika ukumbi wa Ubungo –Urafiki Social
hall.
“Kongamano
hilo litazungumzia maliasili na rasilimali za mkoa wa Rukwa na
maendelao yake ,kiuchumi,kisiasa,kijamii na kiutamaduni nawaomba
wanarukwa wajitokeze na kuhudhuria kwa wingi”alisema bw. Sikulumbwe,
Naye
Makamo mwenyekiti kamati ya wahadhiri mchakato wa chuo kikuu cha Rukwa
bw.Bernard Kasimila amesema sababu ya kuanzisha chuo hicho ni kuwezesha
vijana wenye sifa za kuendelea na masomo kupata fursa ya kujiunga na
chuo kikuu.
Mkoa
wa Rukwa ni sehemu ya Tanzania iliyoko nyanda za juu kusini yenye
wakazi zaidi ya milioni moja kwa sense ya 2012 , una wilaya 3,
halmashauri 4,tarafa 17,kata 64,na vijiji 202,unajishughuli zaidi na
kilimo,uvuvi na utalii.
0 comments:
Post a Comment