Mhandisi Stella
Manyanya amepanga kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa ardhi mkoani
humo ambao wamekuwa wakiuza maeneo ya wazi yaliyotengwa kwaajili ya shughuli
mbalimbali za kijamii.
Hatua hiyo
inafuatia baadhi ya maafisa ardhi hususan katika Manispaa ya Sumbawanga ambao
wamekuwa wakilalamikiwa kubadilisha matumizi viwanja vya wazi vilivyotengwa
huku wakigubikwa pia na tuhuma rushwa ktk mamlaka zao.
Akizungumza
na chemba ya Wafanyabiasha na Wakulima (TCCIA) mkoani Rukwa, Mh. Manyanya
amesema sekta ya viwanda na biashara inashindwa kupiga hatua kwa haraka
kutokana na moja ya kikwazo cha wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa huo kukosa
maeneo ya kuwekeza ambapo yale yaliyotengwa yanavurugwa na baadhi ya maafisa ardhi
wenye tamaa ya kupata fedha kwa njia zisizo halali.
Amewatahadharisha wataalamu hao kubadili mienendo yao kwa kuzingia maadili ya kazi zao na kuachana na tamaa ya kuuza maeneo yaliyo wazi.
0 comments:
Post a Comment