Mwenge huo wa
Uhuru umetembelea miradi 23 ya maendeleo na miradi 28 ya vikundi Mkoani
Rukwa vyenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni
3.4 ikiwa ni mchango wa Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau
wengine wa maendeleo.
Ndege
ndogo ya Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipaa angani katika
uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo tarehe 23 Julai 2013 ikiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, wakimbiza Mwenge wa Uhuru
kitaifa sita pamoja na Mwenge wa Uhuru utakaoenda kukabidhiwa Mkoani
Tabora na Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa. Wakimbiza mwenge hao ni Ndugu Juma
Ali Simai (Kiongozi), Zamda A. John, Christopher Emmanuel, Seperatus
Lubinga, Zuwena Abdallah na Mgeni S. Mgeni.
Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhandisi Stella Manyanya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukamilisha
ratiba yake katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo wa
Mkoa atasafiri kwa ndege kuukabidhi Mwenge huo Mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya kuwaaga wakimbiza
mwenge kitaifa na Mwenge wa Uhuru muda mfupi kabla ya kusafiri na
Mwenge huo kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Tabora mapema leo tarehe 23
Julai 2013. Katika hotuba yake hiyo aliwapongeza wakimbiza Mwenge wote
na wananchi Mkoani Rukwa kwa kufanikisha zoezi hilo kikamilifu na kuwapa
vyeti vya pongezi wakimbiza Mwenge hao wa kitaifa.
Picha
ya pamoja kati ya kikundi cha matarumbeta kilichokuwa mstari wa mbele
katika kutumbuiza kwenye ziara ya Mwenge Mkoani Rukwa na baadhi ya
wakimbiza Mwenge kitaifa na mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu
Abubakari Serungwe wa kwanza kulia (mbele).
Kiongozi wa
mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizungumza na wananchi wa
Manispaa ya Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi Mjini Sumbawanga
tarehe 22 Julai 2013. Kulia ni Diwani wa kata ya katandala Ndugu
Kisabwite na Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
Mkuu wa
Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kmanta akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo
Moshi Chang’a Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani
humo tarehe 20 Julai 2013.
Mkuu wa
Wilaya ya Kalambo machachari katika mbio za mwenge wa Uhuru Moshi
Chang’a akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka Mwenge
wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Kalambo tarehe 21
Julai 2013
Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga Methwew Sedoyyeka akipokea mwenge wa Uhuru kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a tarehe 21 Julai 2013 na
kuahidi kuukimbiza katika wilaya yake kwa amani, nguvu na uadilifu
mkubwa.
Baadhi ya raia wa kigeni nao waliomba kupiga picha na Mwenge wetu wa Uhuru.
Wananchi na
wanafunzi walihamasika vya kutosha na Mwenge wa Uhuru kiasi cha wengine
kupanda juu ya miti ili waweze kupata taswira yake mwanana.
Wanafunzi na wananchi wakiwa juu ya miti kushuhudia Mwenge wa Uhuru na ujumbe wake.
Kwa wengine kuuona Mwenge wa Uhuru vizuri haikuwa kazi rahisi walilazimika hata kuhatarisha maisha yao.
Picha ya
pamoja kati ya mratibu wa Mwenge Mkoani Rukwa ndugu Abubakar Serungwe na
baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa pamoja na katibu wa CCM Sumbawanga
Mjini Mama Silaf Maufi.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa “rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment