Home » » MKUTANO WA MAHAKIMU WAFAWIDHI KANDA YA MAHAKAMA KUU SUMBAWANGA

MKUTANO WA MAHAKIMU WAFAWIDHI KANDA YA MAHAKAMA KUU SUMBAWANGA


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mhe. Kakusulo Sambo akiongoza Mkutano wa Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa ya Rukwa na Katavi. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kubaini, pamoja na mambo mengine, mashauri ya muda mrefu katika kanda na mikakati ya kuyamaliza mashauri hayo. kushotokwake ni Mhe. Jacobs Mwambegele, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga na kulia ni Mhe. Matembele; Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa ya Rukwa na Katavi wakimsikiliza kwa makini Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mh. Kakusulo Sambo (hayupo pichani).
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Mh. Kakusulo Sambo, akiwaonyesha Mahakimu Wafawidhi mikoa ya Rukwa na Katavi fomu maalum inayopaswa kujazwa kila robo mwaka kwa ajili kuonyesha na kubaini kesi za muda mrefu katika mahakama na kisha kuziwekea mikakati kesi zilizokaa muda mrefu katika masijala za Mahakama.
 Picha na Sultani Kipingo-Michuzi blog

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa