Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga
Sumbawanga
POLISI wilayani Sumbawanga
mkoani hapa linamsaka mlinzi
wa Export Trading Company
Ltd , Jofrey Kabungo (35) akituhumiwa kuiba
kiasi cha Sh,
milioni 64 nyumbani kwa Meneja wa
Kampuni hiyo , Kamlesh Patel (46)
.
Kwa mujibu
wa Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani Rukwa , Peter Ngusa Kampuni
hiyo ya Export Trading Company Limited yenye
Makao yake Makuu , Jijini Dar Es Salaam
inamilikiwa na Mohamed Dewji .
Akisimulia kisa cha
wizi huo , Ngusa alidai kuwa
fedha hizo zilikuwa zimehifadhiwa
nyumbani kwa Meneja wa Kampuni hiyo Patel chini
ya meza chumbani kwake
zikiwa zimeviringishwa kwenye kifurushi kwa ajili
ya ununuzi wa ufuta .
Aliongeza kuwa
uchunguzi wa awali
umebainisha kuwa chanzo cha
tukio hilo ni
uzembe wa Meneja
wa Kampuni hiyo
kwa kuacha kifurushi ya fedha
hizo chini ya
meza na kuuacha mlango ukiwa
wazi .
Kwa mujibu wa Ngusa
, mtuhumiwa huyo alifanikiwa kutoroka na kujificha
kusikojulikana mara tu baada ya
kutenda uhalifu huo , licha ya
kumsaka lakini pia Polisi
wanaendelea na uchunguzi
wa tukio hilo .
0 comments:
Post a Comment