MWANAFUNZI wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kipwa mwambao mwa
Ziwa Tanganyika wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa mwenye miaka
minane ameweza kujiokoa yeye na mtoto wa dada yake mwenye umri wa miezi
mitano kwa kuogelea hadi ufukweni baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria
kuzama kwenye ziwa Tanganyika.
Manusura huyo aliyefahamika kwa
jina moja la Prisca akiwa miongoni mwa wengine 15 walinusurika kufa maji
ama kwa kuogelea au kuokolewa alipoona mtumbwi huo ukizama, inadaiwa
alipiga mbizi majini akiwa na mtoto huyo mchanga mgongoni mwake na
kuweza kuogelea kwa saa kadhaa hadi ufukweni wote wakiwa hai.
Kaimu
Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kipwa katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ,
Benson Silinjile alithibitisha mkasa huo wa aina yake akisema msichana
huyo Prisca alikuwa amempeleka mtoto huyo kupata chanjo katika kituo cha
afya kijijini Kapele kwa kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa mgonjwa hivyo
alimwomba msaada huo.
Licha ya msichana huyo kuweza kujiokoa yeye
na mtoto huyo mchanga kwa kuogelea hadi ufukweni pia nahodha wa mtumbwi
huo uliopata ajali hiyo iliyosababisa vifo vya watu 13 wakiwemo wanawake
na watoto wenye umri chini ya miaka mitano , Lazaro Sikapote (26)
aliweza kuokoa familia yake akiwemo mama yake mzazi Rose Sikapote ,
mkewe Rakadia Sikazwe na mwanae aliyefahamika kama Nazaro Sikapote.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment