Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na umoja wa makundi ya wafugaji wa Wilayani Nkasi tarehe 10.03.2013 waliounda umoja wao kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Kimanta kwa lengo la kuboresha maisha ya wafugaji na ufugaji Wilayani humo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wafugaji hao kutambuana ili kurasimisha kazi yao pamoja na kuirahisishia Serikali katika kudhibiti uhamiaji holela wa mifugo Mkoani Rukwa. Aliwataka pia kusomesha watoto wao badala ya kuwatumia katika shughuli zao za uchungaji wa mifugo kama ilivyo hivi sasa.
Mwenyekiti wa umoja huo akizungumzia mikakati waliyojiwekea katika kuimarisha ufugaji wa kisasa wenye tija na masoko ya uhakika Wilayani Nkasi. Umoja huo utakuwa na lengo kusaidia kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji, kuelimishana na kuwekeana mikakati juu ya ufugaji wa ng'ombe wachache wenye tija, malisho bora, masoko, madawa na majosho, kudhibiti wafugaji wengine wasiotii sheria na kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha na kuendeleza ufugaji wa kisasa nchini.
Baadhi ya wafugaji wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Community Centre Mjini Namanyere tarehe 10.03.2013. Jumla ya wafugaji 150 walitegemewa kushiriki katika kikao hicho. Hata hivyo idadi hiyo haikutimia.
Baadhi ya wa wafugaji na viongozi wa Wilaya ya Nkasi walioshiriki kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema nia ya Serikali yake ni kushirikiana na umoja huo kuhakikisha Wilaya yake inajiimarisha zaidi katika ufugaji wa kisasa na kuendeleza umoja huo ambao una mipango ya kujenga ofisi kubwa na shule ya bweni kwa ajili ya watoto wa wafugaji. Hakusita kuweka wazi kuwa Serikali yake ya Wilaya haitowavumilia wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi (Game Reserves) na kwamba wanatakiwa waondoke mara moja kabla Serikali haijaanza msako wa kuwaondoa ambao unategemewa kuanza muda sio mrefu.
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ali Kessi akizungumza ambapo alisistizia kuhusu ufugaji wa kisasa wa kupunguza mifugo kwa kufuga mifugo wachache wenye tija pamoja na kupambana na wahamiaji haramu wa mifugo.
Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini Deosderius Mipata akizungumza katika kikao hicho ambapo alisemea uhifadhi wa mazingira ikiwepo utunzaji wa hifadhi ya akiba ya Lwafi Game Reserve ambayo imeshaanza kuvamiwa na wakulima na wafugaji.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kwela na Mwanasiasa nguli nchini Ndugu Chrissant Majiyatanga Mzindakaya akishukuru kwa niaba ya wafugaji wenzake wa Wilaya ya Nkasi katika kikao hicho. Ndugu Mzindakaya ambaye pia ni Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha nyama Afrika ya Mashariki alielezea fursa kubwa ya masoko ambayo ipo kwa ajili ya wafugaji hao na kusisiktiza juu ya ufugaji bora kufaidi soko hilo.
Bwana Amidi Baraka Magasha Mfugaji wa Kitalu namba 55/15 Kalambo Ranch akiwasilisha hoja yake katika kikao hicho ambapo aliiomba Serikali kushirikiana kwa karibu na wafugaji kwa ustawi wa sekta hiyo, Aliiomba Serikali na wafugaji wenzake kuweka kipaombele kwenye uhifadhi wa mazingira hususani moto.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment