Home » » NHC KUJENGA NYUMBA HADI VIJIJINI

NHC KUJENGA NYUMBA HADI VIJIJINI

Wakazi wa vijiji vya mkoa wa Katavi na Rukwa huenda wakaanza kunufaika na mpango wa ujenzi wa nyumba bora na za kisasa zitakazo jengwa  kwenye vijiji vyao na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Nyumba hizo zitakazojengwa na kuuzwa kwa mikopo zinatarajiwa kujengwa kwenye maeneo mbalimbali ya miji midogo yenye mvuto wa kibiashara  na vile vijiji ambavyo baadhi ya wananchi watapeleka maombi ya maalumu ya kujengewa nyumba na NHC.

Akizungumza mpango mpango huo mbele ya madiwani wa mikoa ya Katavi na Rukwa, Meneja wa NHC kwenye mikoa hiyo Nehemia Msigwa amesema tayari Shirika hilo limejipanga kutaka kuayafikia maeneo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na yale ya vijijini iwapo kuna mwananchi ataonesha kuwa na uwezo wa kumudu gharama za kuuziwa nyumba itakayojengwa na  NHC.

Alisema tayari wameanza ujenzi wa zaidi ya nyumba 40 katika eneo la Ilembo mjini Mpanda ambazo zitauzwa kwa watu watakao kuwa tayari na baadhi zitapangishwa kwa watumishi .

Aidha aliwataka Watendaji wa halmashauri kwenye mikoa hiyo kutumia fursa ya kukopa kwewnye taasisi ya kifedha ili kuweza kujenga majengo ya vitega uchumi kwenye maeneo yao.

Hatahivyo Bw. Msgwa amezitaka halmashauri kuandaa mazingira mazuri kwa NHC ikiwa ni pamoja na kupunguza bei za viwanja ili kuweza kujenga nyumba za bei nafuu ambazo wananchi  watazimudu, huku akiongeza kuwa gharama  za  zinategemea pia gharama za ununuzi wa viwanja, bei ya malighafi za ujenzi na hadhi ya nyumba yenyewe.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa