Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akikabidhi cheti kwa
mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya st maurus ya mjini
sumbawanga waksati wa mahafaloi ya 14 ya shule hiyo mwishoni mwa wiki. Picha na
MUssa Mwangoka.
Wanafunzi wa shule ya St Maurus Chemchemi ya mjini Sumbawanga wakiwa kwenye
picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Rukwa,. Stella Manyanya mwishoni mwa wiki
kwenye mahafari ya shule hiyo.
--------------------------------------------

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu
WAKAZI wa mkoa wa Rukwa wametakiwa kubadilika fikra na mitizamo kuhusu suala la elimu na kuanza kuwasomesha watoto ili waweze kumudu soko la ushindani wa ajira na kuepuka kuwa wasindikizaji wa maendeleo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema hayo juzi wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari St Maurus Chemchemi ya Mjini Sumbawanga.
Alisema kuwa ushindani wa ajira uliopo hivi sasa ni mkubwa hivyo wazazi wasipobadilika kuona umuhimu wa elimu sambamba na kutia mkazo kuhusu suala hilo kwa vijana wao upo uwezekano wa watoto wao kuishia kuwa wasindikizaji wa maendeleo.
'upo uwezekano wa vijana wetu kuwa wasindikizaji wa maendeleo kwa siku za usoni hasa ujenzi wa barabara ya lami utakapokamilika, wageni wengi watakuja kuomba ajira na wataajiriwa kama vijana wetu hawatapata elimu ya kutosha yenye kudumu ushindani" alisema Manyanya.
Pia Manyanya aliwataka kuacha tabia ya wanafunzi kuchukua muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kufuatilia mambo yasiyo na msingi kwao na badala yake watumie mitandao hiyo kwa manufaa yao kielimu.
Alisema tangu mitandao ya jamii kama vile facebook na Twitter wanafunzi wengi wantumia muda mrefu kwaajili ya kuzungumza kwa ujumbe wa maandishi (chat) badala ya kuitumia kwa manufaa yao kielimu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa udhibiti wa tatizo la ujauizito kwa wanafunzi wa kike linakuwa gumu kutokana na baadhi ya wazazi kuwaficha wale wanaowapa mimba watoto wao.
Alisema kuwa kamwe hawezi kuvumilia kuona wazazi wanawachifa wahalifu hao na iwapo itabainika wanaendelea kufanya hivyo basi mamlaka husika zitahakikisha zinawakamata ili wasaidie kumpata mtu aliyempachika ujauzito mtoto mtoto wake wa kike na kumkatishia masomo yake.
Awali akisoma risala ya wanafunzi hao wanaohitimu kidato cha nne, Mwanafunzi Kenneth Neoli alisema kuwa ipo haja sasa kwa Serikali kuanza kuzisaidia shule za binafsi kwa kuzipatia vitabu kwa kuwa nazo zina mchango katika kuielimisha jamii.

Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment