Home » » WAANDISHI WAASWA KUANDIKA HABARI ZA VIJIJINI.

WAANDISHI WAASWA KUANDIKA HABARI ZA VIJIJINI.




 Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Rukwa wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijiji. mafunzo hayo yameandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini. (UTPC) kufanyika kwenye ukumbi wa CWT mjini Sumbawanga.

 Waandishi wa habari wakiwa katika makundi wakijadili mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika mafunzo yao ya uandishi wa habari za vijijini leo kwenye ukumbi wa CWT mjini Sumbawanga. mafunzo hayo yameandaliwa na UTPC.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Rukwa, Peti Siyame akichangia mada katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini yanayofanyika mjini Sumbawanga.
-------------------------------------
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

IMEELEZWA waandishi wa habari nchini wana nafasi kubwa ya kusaidia kupunguza umasikini vijijini iwapo watatoa kipaumbelea kwa kuandika na kutangaza habari za maeneo vijijini.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini kutoka klabu ya uandishi wa habari ya mkoa wa Rukwa, Nswima Ernest alisema leo wakati akichangia mada katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa umoja kwa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kushirikisha waandishi wa habari 18 wa mkoa huo.

Nswima alisema kuwa ni jukumu la waandishi wa habari kuyafikia maeneo ya vijijini na kuibua changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini hali ambayo itasaidia kupunguza kupunguza umasikini uliokithiri kwenye maeneo yao.

Aliongeza kuwa vijijini kuna matatizo mengi yanayowakabili wananchi wa vijijini hususani katika sekta ya afya, maji, elimu, miundombinu na kilimo yanaweza kutafutiwa ufumbuzi na Serikali iwapo waandishi watatangaza changamoto hizo.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Said Dogoli alisema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kutambua kuwa wanajukumu kubwa katika kuisaidia jamii hivyo ni jukumu lao kuandika habari za vijijini hasa wakijikita katika kuchambua sera mbalimbali ambazo Serikali imeziweka lakini haizitekelezi kwa manufaa ya wananchi wa vijijini.

Alisema kuwa zipo sera za afya, elimu na kilimo ambazo Serikali imeziweka lakini zinaonekana bado hazina tija kwa wananchi wa maeneo ya vijijini hivyo sasa ni wajibu wa waandishi kuzichambua ili kuikumbusha Serikali na wadau wengine kuzitekeleza hali ambayo itawasaidia wananchi kuondokana na umasikini.

Blogzamikoa

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa