Home » » ‘ACHENI KUHIFADHI PESA KWENYE VIROBA, TUMIENI BENKI’

‘ACHENI KUHIFADHI PESA KWENYE VIROBA, TUMIENI BENKI’



Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akipokea sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru Tanzania bara kutoka Mkurugenzi wa benki kuu kanda Mbeya, Moses Kasabile ambayo ina thamani ya Sh 50,000 kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwake mjini Sumbawanga.


Meneja wa Idara ya uchumi wa Benki kuu kanda ya Mbeya, Allan Tuni akizungumza katika kikao baina ya viongozi wa benki kuu kanda ya Mbeya na uongozi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa. Picha zote na Mussa Mwangoka.
-------------------------------------
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

WAFUGAJI na wafanyabiashara wa mazao mkoani Rukwa, wametakiwa kuachana na tabia iliyojengeka miongoni mwao ya kuhifadhi fedha kwenye viroba na ngozi na badala yake wajenge utamaduni wa kuweka fedha hizo benki.

Meneja wa Idara ya Uchumi wa Benki kuu kanda ya Mbeya, Allan Tuni alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye kikao baina viongozi kutoka benki hiyo na uongozi wa mkoa wa Rukwa kilichofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Alisema kuwa kuweka fedha benki kuna faida nyingi zikiwamo kuwapo kwa bima inayowalinda waekaji na haki zao, hivyo hakuna sababu za msingi za kuwafanya wafanyabiashara kuogopa kuweka fedha zao kwenye taasisi hizo.

"kuna taarifa kuwa huku kuna wafugaji wengi ambao wanahifadhi fedha kwenye viroba na ngozi, sasa waache kufanya hivyo na waanze utamaduni wa kuweka pesa benki kwani hali hiyo itasaidia watu wengine waweze kupata mikopo kutoka kwenye taasisi hizo kifedha hali ambayo itasaidia fedha nyingi kuingia mzunguko' alisema.

Awali, Mkurugenzi wa benki hiyo kanda ya Mbeya, Moses Gasabile alisema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kufungua kituo cha benki hiyo mkoani Rukwa ili wateja wao ambao ni taasisi za kifedha zilizopo mkoani Rukwa na Katavi wasiangaike tena kuzifuata fedha Mbeya kama ilivyo sasa.

Mkurugenzi Gasabile alisema kuwa licha kutumia gharama kuzifuata fedha Mbeya lakini tatizo jingine linalojitokeza ni kutorudhishwa kwa fedha za noti na sarafu chakavu kutokana na umbali uliopo hali ambayo inasababisha kuadimika kwa sarafu hivyo uwepo wa kituo hicho mkoani humo kumaliza tatizo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema kuwa ipo haja ya kufikia mahali kwamba kilimo chetu kitoe thamani ya kazi inayofanywa na wananchi.

Alisema kuwa ikiwezekana katika kudai wanazuia mfumuko wa bei, benki hiyo itoe fedha ya kutosha ili kununua chakula kwa wakulima wa mkoa huo kwa bei inayostahili badala ya kununua nje ya nchi tena kwa bei kubwa zaidi kwani kufanya hivyo ni kutowatendea haki wakulima.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa