Home » » MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MKOANI RUKWA

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA MKOANI RUKWA

 Mkazi mmoja wa Bangwe mjini Sumbawanga akipita kando ya barabara ya Msakila huku akisaidiana na mtoto ambaye haikufahamika mara moja kama ni mtoto wake, kusukuma baiskeli iliyobeba mzigo wa miwa wakielekea sokoni kwa ajili ya kuuza bidhaa hiyo.
 Wauzaji wa vitunguu wakiwa wamepanga bidhaa zao chini huku wakisubiri wanunuzi jana kwenye eneo la sendi ya daladala ziendazo majengo mjini Smbawanga.


 

Wakazi wa eneo la Majengo mjini Sumbawanga, wakiwa katika foleni ya kuomba msaada wa kuchota maji katika nyumba ya mtu mmoja ambaye uhifadhi maji kwenye matenki makubwa.
 Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akipokea sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru Tanzania bara kutoka Mkurugenzi wa benki kuu kanda Mbeya, Moses Kasabile ambayo ina thamani ya Sh 50,000 kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwake mjini Sumbawanga.
 Meneja wa Idara ya uchumi wa Benki kuu kanda ya Mbeya, Allan Tuni akizungumza katika kikao baina ya viongozi wa benki kuu kanda ya Mbeya na uongozi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa.
 Mkurugenzi wa Shirika la JHPIEGO nchini Tanzania, Maryjane Lacoste akizungumza katika kikao baina ya wataalamu wa Shirika hilo, Africare na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Stella Manyanya hayupo pichani jana ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa.
 Mwandishi wa habari, Mussa Mwangoka akiangalia baadhi ya pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya matumizi ya akina mama wajawazito zilizohifadhiwa katika jengo la Manispaa ya Sumbawanga, tangu Serikali itoe pikipiki kwa uongozi wa Manispaa hiyo zina zaidi ya mwaka mmoja sasa zikiwa hazijaanza kutumika. 
Picha zote na Mussa Mwangoka-Rukwa Yetu
Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa