Home » » UNUNUAJI VIFAA VYA KUJIFUNGULIA WAWATESA NKASI

UNUNUAJI VIFAA VYA KUJIFUNGULIA WAWATESA NKASI

na Mwandishi wetu, Nkasi
DHANA ya Serikali ya kuwataka kina mama wajawazito kutonunua vifaa wakati wa kujifungua, inaonekana kushindwa kutekelezeka kivitendo hasa katika maeneo ya pembezoni mwa nchi kutokana na vifaa hivyo kutopatikana kwa wakati katika vituo vya afya.
Hayo yalisemwa na Mganga Msaidizi wa Kituo cha Afya cha Kirando, Wilayani Nkasi, Dk. Wilinard Msinjili, katika mahojiano maalum na gazeti hili.
Dk. Msinjili alisema, jambo hilo linawapa wakati mgumu pindi wakina mama wanapofika kituoni hapo wakiwa hawana vifaa, jambo linalowafanya wahudumu kuchangishana fedha kwa ajili ya kuokoa maisha ya kina mama hao.
Hata hivyo, pamoja na matatizo hayo, Dk. Msinjili alisema kina baba wa Wilaya hiyo kwa sasa tangu wapate elimu kupitia mradi wa ushiriki wa wanaume katika afya ya uzazi (TMEP), wamekuwa wakinunua vifaa hivyo mapema kuhakikisha wake zao wanajifungua salama.
“Hili tatizo, kwa kweli Serikali inabidi kulingalia kwa jicho la karibu, kwa kuwa tulioko huku vijijini ndio tunaoshuhudia, wasisubiri kupelekewa ripoti za makaratasi, ndio maana suala la wahudumu kuuza vifaa hivyo hospitalini, halitakoma,” alisema.
Akilizungumzia tatizo hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Emmanuel Kushoka, alisema kushindwa kupatikana kwa vifaa katika vituo vya afya kwa kiasi kikubwa kunasababishwa na Bohari ya Madawa (MSD), ambayo hushindwa kupeleka dawa hizo kwa wakati.
Aidha, Kushoka alisema hata pale wanapopitisha bajeti ya Wilaya, mara nyingi fedha walizoziomba hazifiki kama zilivyo, hivyo kukwamisha mipango mingi katika idara nzima ya afya.
Chanzo: Tanzania Daima
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa