Home » » DC ATANGAZA KIAMA KWA WATAKAOHUJUMU SENSA

DC ATANGAZA KIAMA KWA WATAKAOHUJUMU SENSA

 
Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sodeyeka, akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa Sensa ya watu na Makazi kilichowashirikisha madiwani hao na kufanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo leo Picha na Mussa Mwangoka.  
 
Baadhi ya Madiwani wa kata zilizopo Manispaa ya Sumbawanga, wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kuhusu sensa ya watu na Makazi katika kikao cha wadau hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa leo Picha na Mussa Mwangoka. 
 
Baadhi ya Madiwani wa kata zilizopo Manispaa ya Sumbawanga, wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kuhusu sensa ya watu na Makazi katika kikao cha wadau hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa leo.Picha na Mussa Mwangoka. 
 
Diwani wa kata ya Majengo mjini Sumbawanga, Vareliana Kalyalya akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa Sensa ya watu na Makazi kilichowashirikisha madiwani hao na kufanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo leo. Picha na Mussa Mwangoka. 

Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Sumbawanga wakifagia barabara ya kuelekea jengo la ofisi za Manispaa hiyo jana ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Sumbawanga Ng'ara. Picha na Mussa Mwangoka.

Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

UONGOZI wa Serikali wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, umesema hautasita kuwachukulia hatua za kisheria kikundi au baadhi ya watu watakaobainika kuharibu kwa makusudi zoezi la upatikanaji wa takwimu za sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika agosti 26 nchini kote.

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sodeyeka alisema hayo (leo) wakati akifungua mafunzo ya Sensa ya watu na Makazi kwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Alisema kuwa zipo taarifa ya kuwapo kwa kikundi cha watu ambacho kimelenga kuharibu zoezi la sensa ya watu na makazi kitu ambacho kitasababisha kutokupatikana kwa takwimu sahihi hali ambayo ni kinyume na malengo ya kufanyika kwa zoezi hilo.

"nimesikia wapo baadhi ya watu wanalenga kuharibu zoezi hili kwa kukataa kuhesabiwa na kutoa taarifa muhimu zinazohitajika...... sasa naomba madiwani tusaidiane kuwatambua ili sheria ichukue mkondo wake, kamwe hatuwezi kuwavumilia watu hao, hiyo ndio tahadhari yangu kwao" alisema mkuu huyo wa wilaya.

Aliongeza kuwa zoezi hilo halina uhusiano wowote na masuala ya itikadi za dini au kisiasa na kuwataka wananchi kuwapuuza wanaopinga kuhesabiwa kwa sababu hizo ukizingatia kwamba lengo la kufanyika kwa zoezi hilo ni kupata takwimu sahihi ambazo hutumika katika sehemu mbalimbali ikiwemo serikalini, taasisi za kimataifa na kutekeleza mipango mbalimbali ya kitaifa inayolenga kuliletea taifa maendeleo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Majengo, Vareliana Kalyalya alisema kuwa zoezi hilo liweze kupata ufanisi ipo haja kwa waandaji kutoa elimu kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji kabla ya siku ya kuanza kwa zoezi hilo muhimu.

Diwani huyo, alisema kuwa watu hao ni muhimu kwa kuwa wanawafahamu watu wanaoishi kwenye maeneo yao na wanaweza kusaidia kutoa ushirikiano mkubwa kwa makarani pindi watakapopita kwenye maeneo hayo ili kupata takwimu za sensa ya watu na makazi.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa