Home » » MAKARANI WALEVI WATAHARIBU ZOEZI LA SENSA

MAKARANI WALEVI WATAHARIBU ZOEZI LA SENSA


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

IPO hatari ya kutopatikana kwa takwimu sahihi iwapo baadhi ya makarani wa Sensa ya Watu na makazi katika wilayani Kalambo mkoani Rukwa wataendekeza ulevi imeelezwa hapa jana.

Katibu Tawala wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Florence Mtepa alisema hayo kwa nyakati tofauti wakati akifunga mafunzo ya makarani wa sensa ya taifa ya watu na makazi yaliyofanyika katika tarafa za Matai, Kasanga na Mwimbi.

Mtepa alisema kuwa  iwapo makarani walioteuliwa kusimamia zoezi hilo watajihusisha  na  ulevi  wakati wa zoezi hilo litakaloanza Agosti 26 mwaka huu upo uwezekano wa kutopatikana kwa takwimu sahihi ambazo taifa linazihitaji katika kupanga mipango yake ya maendeleo.

 “Kumbukeni mtakuwa pekee yenu katika maeneo ya sensa mlikopangiwa, hivyo lazima mtumie hekima zenu ili kufanikisha zoezi  hilo, ukizingatiwa kuwa mmepewa dhamana kubwa katika taifa hili” Alisema Mtepa.

Alisema zoezi hilo la sensa limetumia fedha nyingi hadi kukamilika kwake , hivyo taifa linahitaji kuona gharama zilizotumika zinatoa tija kwa serikali badala ya zoezi hli kuharibiwa na watu wachache wasiolitakiwa mema taifa.

Mtepa alisema hamasa kubwa imekwisha fanyika kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa kijamii na wa kidini na mwelelekeo unaonekana kuwa mzuri kwa watu wengi kusubiria kuhesabiwa katika kaya zao.

Alisema……“Hata yale madhehebu ya dini kama vile’ Watch Tower’ tumezungumza nao na wamekubali kuhesabiwa na wanatupa ushirikiano wa kutosha kwa kuwahamasisha waumini wao katika zoezi hili la sense”.

Mafunzo ya Makarani wa sensa katika wilaya ya Kalaombo yamefanyika huku waratibu wakithibitisha kupata na kuvitawanya   kwenye taarifa tatu tofauti ambazo ni Matai, Kasanga na Mwimbi.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa