Home » » MABADILIKO YA TABIA NCHI YATISHIA RUKWA.

MABADILIKO YA TABIA NCHI YATISHIA RUKWA.

 Katibu Mtendaji wa muungano wa asasi zisizo za Kiserikali mkoani Rukwa, Stanley Mshana akitoa mada jana kwenye mdahalo wa kuelimisha wananchi wa kijiji cha Mwazye kuhusu mabadiliko ya Tabianchi. Picha na Mussa Mwangoka.


 
Baadhi wa wakazi wa kijiji cha Mwazye wakifuatilia kwa makini mdahalo kuhusu mabadiliko ya tabianchi uliofanyika kwenye ofisi za kata ya Mwazye jana. picha na Mussa Mwangoka.
Mjumbe wa bodi ya muungano wa asasi zisizo za Kiserikali mkoani Rukwa, Josepha Michese akitoa mada jana kwenye mdahalo wa kuelimisha wananchi wa kijiji cha Mwazye kuhusu mabadiliko ya Tabianchi. Picha na Mussa Mwangoka.

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu.

WANANCHI  wa Mkoa wa Rukwa, wametakiwa kuacha kuharibu  mazingira  ili   waweze  kuepukana  na  athari  kubwa  ya mabadiliko  ya tabia  nchi   kama  ilivyo katika   nchi nyingi  za magharibi.

Katibu Mtendaji wa muungano wa Asasi zisizo za Kiserikali Mkoani Rukwa (Rango), Stanley Mshana alitoa tahadhari hiyo jana kwa wananchi wa kijiji cha Mwazye kata ya Mwimbi wilayani Kalambo, wakati akitoa mada kwenye mdahalo wa kuelimisha wananchi kuhusu mabadiliko ya Tabianchi uliofadhiliwa na shirika la Civil Society for Foundation.

Alisema  kuwa  mabadiliko ya tabia nchi yanayotokea hivi sasa nchini ni matokeo ya uharibifu wa mazingira, ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilima katika vyanzo vya maji, ukataji wa miti na uchomaji ovyo wa misitu.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maeneo yamekuwa na ukame, joto limeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma, kitu ambacho kamwe hakiwezi kufumbiwa macho hivyo ni wajibu wa wananchi kuchukua tahadhari na kuacha kuharibu mazingira.

Alisema kuwa ili kuhakisha  wanadhibiti  hali   ya uhalibifu  wa   mazingira katika  maeneo  yao hawana budi kupanda   miti  na kutoruhusu  ukataji  holela  na  uchomaji  moto   ovyo  wa  misitu kama   ilivyo  hivi  sasa.

Naye Mjumbe wa bodi ya Asasi hiyo, Josephat Michese, alisema licha ya mkoa wa Rukwa ambako athari za mabadiliko ya tabia nchi si kubwa sana lakini katika baadhi ya mikoa zimeanza kuonekana ambapo ugonjwa wa malaria umeenea kwa kasi kwenye maeneo ambayo haukuwa wa kawaida kama vile Amani (Tanga), Mpwapwa, Lushoto, Rungwe, Njombe, Mufindi na Muleba kutokana na mabadiliko ya jotobaridi.

Alisema kuwa Wilaya ya Hanang na Babati zimepata milipuko ya Malaria kutokana na ukame ambao pia umesababisha utapiamlo na upungufu wa kinga na uwezo wa kuhimili magonjwa kitu ambacho si kizuri kutokea katika mkoa wa Rukwa hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kabla hali kama hiyo haijatokea.

Blogzamikoa


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa