Home » » PICHA ZA WIKI KUTOKA MKOANI RUKWA

PICHA ZA WIKI KUTOKA MKOANI RUKWA

 Baadhi ya wasichana wakazi wa kijiji cha Kisumba Kasote wakiwa wamebeba vikapu ambavyo ndani yake kuna mihogo wakielekea mashineni kugasa kwaajili ya kupata unga wa muhogo ambao hutumiwa zaidi kwaajili ya kutengezea chakula aina ya ugali katika eneo hilo. Picha na Mussa Mwangoka.  
 Mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Rukwa Social Services Organization (RUSOSEO), Dk. Peter Lenyelele akisoma taarifa ya asasi hiyo jana kwa mgeni rasmi ambaye ni mratibu wa Tacaids Mkoa wa Rukwa Daniel Mwaiteleke (hayupo pichani)  katika uzinduzi wa mradi wa Mapambano dhidi ya ukimwi katika kata ya Kisumba Kasote uliofadhiliwa na Geita Gold Mining. Picha na Mussa Mwangoka.
Mratibu wa Tacaids Mkoa wa Rukwa Daniel Mwaiteleke, kushoto akikabidhi baadhi ya vipeperushi kwa diwani wa kata ya Kisumba Kasote, Paul Kasitu jana baada ya uzinduzi wa mradi wa Mapambano dhidi ya ukimwi katika kata ya Kisumba Kasote uliofadhiliwa na Geita Gold Mining. Picha na Mussa Mwangoka.
Blogzamikoa

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa