Home » » AMUA MKE MWENZA KWA KUMKATA MAPANGA

AMUA MKE MWENZA KWA KUMKATA MAPANGA

Mussa Mwangoka, Sumbawanga.
JESHI la Polisi mkoa wa Rukwa, linamshikilia Debora Sasile (25) Mkazi wa kijiji cha Korongwe, tarafa ya Kirando, wilayani Nkasi kwa tuhuma ya kumuua kwa kumkatakata mapanga mke mwenzake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea agosti 2 mwaka huu saa 11 jioni katika kijiji cha Korongwe, na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Juliana Kazinda (37).
Kamanda Mwaruanda alisema siku ya tukio wanawake hao wawili ambao ni wake wa Ismail Simbi (40) wakiwa nyumbani kwa Juliana walianza kugombana kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Inasemekana kuwa  Debora ambaye ni mke mdogo alitoka nyumbani kwake na kumfuata mwenzake na kuanza kumtuhumu kuwa ni mchawi na anamfanyia dawa mume wao ili amuache yeye mke mdogo, tuhuma hizo ziliisababisha kutokea kwa ugumvi baina yao na kusababisha mtuhumiwa kujeruhiwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, Juliana alijeruhiwa mwili, mikononi na tumboni ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu  katika kituo cha afya cha Kirando ambako alikuwa amelazwa, ambapo mtuhumiwa bado anahojiwa na polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.
Katika tukio jingine, Kijana Frolence Malizia (34) amefariki dunia wakati alipokuwa anafukuzwa na askari mgambo pamoja na wananchi kufuatia kutoroka mahakamani wakati mahakama ikiendelea.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, tukio hilo lilitokea julai 31 mwaka huu saa nne asubuhi katika mahakama ya mwanzo ya Laela Wilayani Sumbawanga wakati mtuhumiwa akisubiri kusomewa mashtaka ya kutishia kuua kwa maneno huku akiwa chini ya ulinzi wa askari mgambo Innocent John (36).
Inadaiwa kuwa wakati wakiwa eneo hilo, kijana huyo aliruka ukuta wa mahakama na kuanza kukimbia hali iliyosababisha askari huyo aanze kumkimbiza huku akipuliza filimbi za kuomba msaada na ndipo wananchi wengi walipojitokeza na kuanza kumfukuza.
Inaelezwa kuwa baada ya kukimbizwa umbali mrefu, mwanaume huyo aliishiwa pumzi na kuanguka chini na kufariki dunia papo hapo.
Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ambapo uchunguzi taarifa ya uchunguzi wa Daktari unahitajika kubaini kilichomuua kijana huyo.
Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa