Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akiwa na mkuu wa wilaya ya Kalambo, Moshi Chang'a kushoto sambamba na aliyekuwa Meneja wa TRA mkoa wa Rukwa Augustino Mukandara katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kuamishiwa mkoa wa Kigoma. ilifanyika jana kwenye ukumbi wa Upendo View mjini Sumbawanga.
Baadhi ya wageni walioalikwa kwenye hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa meneja wa TRA mkoa wa Rukwa baada ya kuamishiwa mkoa wa Kigoma, ilifanyika jana kwenye ukumbi wa Upendo View mjini Sumbawanga.
Mussa Mwangoka, Sumbawanga. Rukwa yetu Blog
WAFANYABIASHA wa mkoa wa Rukwa wametakiwa kuachana na dhana zilizojengeka miongoni mwao kuwa wawekezaji ni wageni kutoka nje ya nchi pekee, badala yake wajitambue na kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa ya ukanda wa ziwa Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema hayo alipokuwa akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkaribisha Meneja mpya wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Philipo Kimune na kumuaaga Augustino Mukandara aliyehamishiwa Mkoani Kigoma ambapo ilifanyika jana kwenye ukumbi wa Upendo uliopo mjini hapa.
Alisema kuwa wafanyabiashara wazawa wana fursa kubwa ya kuwekeza katika mkoa huo kuliko wageni hivyo nao wanapaswa kuzichangamkia fursa za uwekezaji zinazotangazwa katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
Manyanya alisema kuwa zipo fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwamo madini,utalii na Kilimo katika mikoa hiyo ambazo wafanyabiashara wanapaswa kuwekeza kwenye maeneo hayo hali ambayo itasaidia kupatikana kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
Aliwataka wafanyabiashara hao kuachana na tabia ya kukwepa kulipa kodi kwani kufanya hivyo kunachangia mkoa na taifa kukosa mapato yanayotokana na kodi hivyo kusababisha mkoa kutopiga hatua kimaendeleo.
"maendeleo sehemu yoyote duniani yanatokana na kodi ........ sasa wafanyabiashara ni lazima walipe kodi kwa mujibu wa sheria na ndipo Serikali inaweza kuwaletea wananchi maendeleo endelevu kwenye sekta mbalimbali zikiwamo za huduma za kijamii" alisema Manyanya.
BLOG ZA MIKOA
0 comments:
Post a Comment